Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Aisee..kwa umri sijawa ila ninakumbuka nikiwa mdogo kama darasa la tano hivi, tulikuwa tunasafiri na gari la kampuni, tufika kwenye daraja flani niliona watoto kama watano hivi wanavheza ule mchezo wa kitoto unaitwa Ukuti ukuti wa mnazi..( Watoto wa leo wanaonyoa viduku hawawezi kujua mchezo huu, wao wanajua kubeti)..
Pale ruvu kwenye saa 8 usiku niko moto bati,ghafla mbele yangu kama mita 30 nikamuona mmama yuko katikati ya barabara nikamkwepa, jamaa niliokua nao kwenye walikua wamepitiwa na usingizi,gari ilivyoyumba wakaamka kwa mshtuko kwa jinsi gari ilivyoyumba, kuniuliza imekuwaje nikawaambia kuna mama alikua kati ya barabara nimemkwepa.

Jamaa wakaanza kunilaumu eti nisingemkwepa,ile safari tulikua tunatoka kucheck match ya Yanga so kulikua na gari zingine nyuma huko za jamaa zetu,baada ya kama dk 10 kuna jamaa walikua nyuma wakatupigia kuuliza tuko wapi na kama tumemuona mmama pale ruvu yuko barabarani!nikawaambia washkaji kama yule ni jini wa nyuma yetu wasingemuona.

Labda tu mama wa watu hayuko sawa tu kiakili,muda mwingine tukiwa barabarani tusiwe tunafikiria negative tu
 
LED tu za gari from 2014 hivi. Niliexperience kwenye Navara ya 2017 aisee taa inapiga mbali kama mchana.
Kweli. Na LED, adaptive na bending lights kwa baadhi ya gari ndizo zinanipa mzuka wa kutafuta njululu ili kupata chuma cha kuanzia miaka hiyo.


Hii teknolojia inapunguza tatizo la kuumiza watumiaji wengine wa barabara.
 
Unawasha indicator ya upande wa kulia kuonyesha mwisho/mpaka wa gari lako.
Hata ukiwasha akishakupiga hio mitaa yake unakuwa huoni kwa sekunde kadhaa. Kama kuna Lori au gari imeachwa barabarani unalivagaa.

Ndio maana inashauriwa ukipishana na mtu usiku punguza mwendo. Kuwasha taa,indicator inasaidia kujua anaekuja Yuko alert/hajalala? Akijibu unajua Yuko alert ukiona hajibu jiandae anaweza kuwa kasinzia.
 
LED tu za gari from 2014 hivi. Niliexperience kwenye Navara ya 2017 aisee taa inapiga mbali kama mchana.
Kuna siku tulikuwa tunasafiri usiku kwenye GLE ya 2017.

Taa zinapiga mpaka mita 700.

Hata ukiwasha full unayepishana nae haumii macho. Kuna cells zinajizima upande wake ila upande mwingine zinaendelea kupiga.
 
Back
Top Bottom