Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kuna mashimo tu na ile migogongo ambayo inaharibu show ipo hasa mlandizi chalinze.. ila matuta naona kama yamekuwa madogo unayafukia na ukijua sehemu zenye mashimo kuna mda unatembea na 160kph tu 🙂🙂.. nilipoteza mda mlandizi baada ya kuona wakuda, ila nilipo imaliza pale mwendo wangu ulikuwa 160, narudi 140 na maeneo machache kwenye ukaguzi kama sehemu tatu nikakopeza mda.. nikakuta inefika masaa manne na nusu
 
Hiyo “migogongo” ndiyo ile mibonyeo? Aisee hiyo hata maeneo kabla na baada ya Gairo ipo. Siipendi kabisa hiyo.
 
Je, kuna aliyekutana na mauzauza barabarani yeye mwenyewe siyo kwa kuhadithiwa?

Iwe kwa safri za usiku ama mchana.
Aisee..kwa umri sijawa ila ninakumbuka nikiwa mdogo kama darasa la tano hivi, tulikuwa tunasafiri na gari la kampuni, tufika kwenye daraja flani niliona watoto kama watano hivi wanavheza ule mchezo wa kitoto unaitwa Ukuti ukuti wa mnazi..( Watoto wa leo wanaonyoa viduku hawawezi kujua mchezo huu, wao wanajua kubeti)

Nilishikwa na kigugumizi, sikuweza kusema chochote gari lilipopita sikusikia kishindo cha mtu kugongwa, nilipotazama nyuma sikuona chochote..
Tulikuwa tumekaa kwenye tela ya pickup..

Hicho nilichokiona sijui ndiyo mauza uza ya barabarani, sijui nilikuwa naota... mpaka leo najiulizaga ni nini kile..

Juzi kati nikapita eneo hilo peke yangu saa nne usiku naendesha gari... nikakumbuka yale niliyowahi kuyaona. niliogopa sana lakini sikuona kitu..
 
Unadhani huyu alikuwa anaenda speed ngapi?View attachment 1775511
Huyo alikuwa anatembea kati ya 140-150kph. Hapo hata gari ingekuwa na airbag 10 huchomoki. Usiku labda uwe umefunga LED sports light ndio utaweza tembea hizo speed, vinginevyo ni bora utembee mwendo wa mateka 80kph au upambane na vibao vya 50 mchana.
 
Huyo alikuwa anatembea kati ya 140-150kph. Hapo hata gari ingekuwa na airbag 10 huchomoki. Usiku labda uwe umefunga LED sports light ndio utaweza tembea hizo speed, vinginevyo ni bora utembee mwendo wa mateka 80kph au upambane na vibao vya 50 mchana.
LED sport ligt zinapiga umbali wa mita ngapi ? nije nizifunge hizi nione mtiti wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…