Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kama ulikuwa na tyre spare hakukuwa na haja ya kutuma mafundi toka dar.

Ungetafuta kijana maeneo ya karibu akusaidie kazi unampa 5000 ya supu.
 
S.O.S 101.
 
Mimi pia naamini hili. Kuwa asipovaa miwani na kama kweli ana shida siku zinavyoenda shida itaongezeka.
 
Kuna mshkaji wangu ana carina yake, idadi ya spares zilizo kwenye gari yake anaweza akafungua micro garage sehemu.

Hadi extra battery anayo. Kila aina ya set ya spana anazo.

Na kazi zote anafanya yeye kwenye gari yake.
Duh hadi spare battery, ndio naiona leo hii.

Itakuwa alikutana na majanga huko kabla. Watu wengine unakuta hana hata spare tyre wala wheel spanner.

Tunatofautiana sana.

Nilishapasukiwa tyre njiani baada ya kufunga spare tyre kabla sijafika sehemu naweza kupata nyingine nilikuwa sina raha kabisa maana najiona kabisa namiss kitu.
 
Kwa jinsi ninavyopenda kuendesha.

Huwa siwi comfortable kukaa pembeni mtu aniendeshe.

Labda nikifika miaka 80 huko (kama ntafika) ndo ntakuwa naendeshwa.

Otherwise, wacha nipige gear.
 
Wenzio uchumi wa kati tunaufurahia kwa kuchoma wese na kutembea vibati. Ni starehe pia.
"Fast driving ni addiction" niliwahi ambiwa na mshua.

Na hakuna jinsi ya kuiondoa mpaka siku unapata fatal accident na unapona. Ile experience ndo itakufunza adabu.

Huwa nakumbuka haya maneno mshale ukishaanza kutoboa 190kph.

Narudi 150 kph taratibu.
 
Mara ya kwanza kufungua mlango wa benz nilidhani ni mbovu.

Haufunguki wote, unafunguka kidogo tu. Inabidi utumie nguvu kuusukuma mpaka mwisho.

Milango ya hizi gari zetu unafungua unaenda wenyewe mpaka mwisho.
Ha ha ha ha kuna dada aliniuliza mlango wako mbovu?! Nikamwambia sukuma tu mlango wa mkoloni mzito kidogo!
 
Kwahio na wewe unaona 150kph sio fast? Mwingine hio 150kph atasema subiri fatal accident uone!
 
Itabidi nifanye mpango aisee..miwani inakera sana.
Kwa hapa bongo wapi naweza pata hiyo huduma?

Hapo penyewe last time Dr alinipima akaniambia computer inaonyesha -4..nikamwambia aache utani.
4 sivai mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni teknolojia mpya, sidhani kama imesambaa sana kwa ufanisi.

Nadhani ungecheki na Dr. Agarwals wapo pale Morocco. Labda wameanza kufanya.

Ni delicate procedure ndo maana binafsi sidhani kama ninaweza mpa mtu jicho langu acheze nalo kiasi hiko.
 
Ha ha ha ila gari za siku hizi haziji na spare tyre,wheel spanner wala jack. Zina run flat tyres ambazo inaweza kutembea bila upepo mpaka km80
 
karibu
unaelekea wapi?

sijakataa ila mimi sina uwezo huo aisee
 
Buti limejaa spare ukipiga tuta unazisikia kwa ndani.

Ni yule mtu akipata safari anaondoka saa hiyohiyo.

Hana haja ya kwenda service atafanya mbele ya safari.

Mnaweza mkawa sehemu kama mcity hivi mnapiga story, ukamwambia kuna deal twende mwanza, ana uwezo akaondoka na carina yake bila hata kwenda nyumbani kwake kuchukua hata nguo.

He's the most mobile guy i've ever seen.

Nikaona sababu ya yeye kubeba madude yote hayo.
 
Hivi Holy Man mwaka huu unaweza ukawa umetembea km ngapi?
Maana kama wewe, mimi pia lazima nisafiri kikazi...

Since January nimekula not less than 10000km highway
Paka sasa hivi kwa haraka haraka tokaea January ni zaidi ya 12,000km, kwababu ndani ya mwezi mmoja huwa natembea kati ya 2000km -5000km. Na kuna wakati trip moja tu huwa ninaenda zaidi ya +2000km non stop. Mfano kwa mwezi huu peke yake nimetembea 3,500km .. na leo usiku nakiamsha from Dsm to Tabora then mwanza..
 
Acha tu kuna gari simple tu ya 2013/14 Mercedes E class kama anayoitamani Holy Man ukiigusa unaona kabisa dunia mbili tofauti na gari za 2007 kushuka chini.
Gari yoyote kuanzia 2014 kwa level zetu Bongo ni nzuri sana acha hizo za 2019/20
😂😂😂 mkuu mda si mrefu naanzia kwenye ML350 japo itakuwa ya ofisi.. ila nitanyanyasa kiaina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…