Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mungu wangu!! Hata jinsi ya kuzungusha spanner enyewe sijui, mie najua kudrive na sheria zake, ikitokea tatzo tyuuh bas nimeshaishiwa kila kitu.

Kuna safar 1 nlkua natoka Dar naenda Moro, sasa ile gari ilkua ina tatizo kwenye tyre, wakat huo mie sijui wala mwenye gari hajui, mie huyo nkachukua ndinga kuanza safari, bhana wee kufika chalinze kwa mbele kidogo kuna ka msitu fulan kadogo,
Nkasikia sauti "paaaah" nilishtka kwa woga nusu niaachie usukan, bahat nzuri nilikua mwendo mdogo tena mdogo mno, bas nka control gari ikasimama pemben ya road, nashuka kuchek hivi naona tyre ya nyuma kulia imepancha.

Kisanga sasa sijui A wala Z kuhus ufundi, yaan sijui lolote, [emoji23][emoji23][emoji23] nilichofanya nlikaa tyuuh ndani ya gari afu nkaanza kulia yaan nalia vibaya sielew, baadae nkaona nimpigie muhusika anasema yeye yuko buzy kazin, hawez kuja, bhana wee nilianza kulia tena [emoji23][emoji23][emoji23] nalia tyuuh sielew, kumbe muhusika amewatuma mafundi wawili wanifate,

Baadae kidogo naona gari imepark mbele yangu, wakashka wanaume wawili na vifaa, wakacheki tatizo ndo wakaanza kutengenza na kubadili tyres, ikawa fresh na safar ya Moro ikaishia hapo nkarudi Dar,

Tangu siku hiyo sichukui gari bila kuhakikiwa kuwa ni nzima, maan itakua habari nyingne.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Kama ulikuwa na tyre spare hakukuwa na haja ya kutuma mafundi toka dar.

Ungetafuta kijana maeneo ya karibu akusaidie kazi unampa 5000 ya supu.
 
Usidiriki kutembea usiku. Yani panga safari yako such that giza linapoingia uwe unafika unakoelekea au unalala. Hata kama hujui ufundi, wasafiri wenzio tunaweza kukusaidia, ila tu hakikisha una spare tairi yenye upepo unaotakiwa, wheel spanner na jeki. Na uvikague kila mara unapoanza safari. Pia hakikisha una triangle za usalama, ukipata shida washa hazard na uweke triangle nyuma na mbele ya gari, mita 50 kila upande. Triangle zinapeperushwa na upepo so zigandamize na jiwe zito.

Fungua bonnet na kaa nje ya gari... tukipita tukakuona umekaa kinyonge tutakuuliza kulikoni na kukupa msaada unaowezekana.
S.O.S 101.
 
Kuna optician aliwahi niambia ukiwa na tatizo na usipolifanyia kazi unazidi kufanya tatizo linakuwa kubwa na linaweza athiri hata vitu vingine.

Sawa na gari, ikifa sensor moja na usipotibu tatizo, matatizo mengine yatazidi kujitokeza.

In the mean time, kavae miwani kwanza huku unajipanga kwa option nyingine nzuri zaidi.
Mimi pia naamini hili. Kuwa asipovaa miwani na kama kweli ana shida siku zinavyoenda shida itaongezeka.
 
Kuna mshkaji wangu ana carina yake, idadi ya spares zilizo kwenye gari yake anaweza akafungua micro garage sehemu.

Hadi extra battery anayo. Kila aina ya set ya spana anazo.

Na kazi zote anafanya yeye kwenye gari yake.
Duh hadi spare battery, ndio naiona leo hii.

Itakuwa alikutana na majanga huko kabla. Watu wengine unakuta hana hata spare tyre wala wheel spanner.

Tunatofautiana sana.

Nilishapasukiwa tyre njiani baada ya kufunga spare tyre kabla sijafika sehemu naweza kupata nyingine nilikuwa sina raha kabisa maana najiona kabisa namiss kitu.
 
Kuna siku nimeendesha from Dar to Mwanza mwenyewe non stop (Touarage imesimama kweli kweli 🙂 . Nimefika around saa kumi na mbili jioni.....

Ile nimeingia hotelini.....nikajiuliza maswali mengi..Masanja ndo naanza kuingia uchumi wa kati...halafu nakimbizana na hizi barabara..why lakini? sikupata jibu la kuridhisha.

Aisee from there on..nina kijana wangu Dar....mda fulani alikuwa dereva wa diplomat mmoja. Nikiwa nasafiri mbali ndo anashika usukani. But if its a 500km and less naendesha mwenyewe.

The good news.... huyu dereva anaijua na kuipenda kazi yake haina mfano! Kikubwa kuliko vyote yaani gari inakaa safi mda wotee....mpaka raha! (nachukia sana gari chafu)

Truth is..nikiwa nasafiri nataka niwe free..nichungulie iPad kidogo..kama nina kiu nifungue ka kopo ka Heineken kidogo ilmradi...nifurahie safari yangu.

Hapana hizo trip ndefu na speed nawaachia...aiseee.....nisije katisha maisha yangu kizembe nikakosa raha za uchumi wa kati.....ambazo nimezihangaikia for years!

Pamoja sana wakuu..life is short..lets enjoy but.......responsibly!
Kwa jinsi ninavyopenda kuendesha.

Huwa siwi comfortable kukaa pembeni mtu aniendeshe.

Labda nikifika miaka 80 huko (kama ntafika) ndo ntakuwa naendeshwa.

Otherwise, wacha nipige gear.
 
Wenzio uchumi wa kati tunaufurahia kwa kuchoma wese na kutembea vibati. Ni starehe pia.
"Fast driving ni addiction" niliwahi ambiwa na mshua.

Na hakuna jinsi ya kuiondoa mpaka siku unapata fatal accident na unapona. Ile experience ndo itakufunza adabu.

Huwa nakumbuka haya maneno mshale ukishaanza kutoboa 190kph.

Narudi 150 kph taratibu.
 
Mara ya kwanza kufungua mlango wa benz nilidhani ni mbovu.

Haufunguki wote, unafunguka kidogo tu. Inabidi utumie nguvu kuusukuma mpaka mwisho.

Milango ya hizi gari zetu unafungua unaenda wenyewe mpaka mwisho.
Ha ha ha ha kuna dada aliniuliza mlango wako mbovu?! Nikamwambia sukuma tu mlango wa mkoloni mzito kidogo!
 
"Fast driving ni addiction" niliwahi ambiwa na mshua.

Na hakuna jinsi ya kuiondoa mpaka siku unapata fatal accident na unapona. Ile experience ndo itakufunza adabu.

Huwa nakumbuka haya maneno mshale ukishaanza kutoboa 190kph.

Narudi 150 kph taratibu.
Kwahio na wewe unaona 150kph sio fast? Mwingine hio 150kph atasema subiri fatal accident uone!
 
Itabidi nifanye mpango aisee..miwani inakera sana.
Kwa hapa bongo wapi naweza pata hiyo huduma?

Hapo penyewe last time Dr alinipima akaniambia computer inaonyesha -4..nikamwambia aache utani.
4 sivai mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni teknolojia mpya, sidhani kama imesambaa sana kwa ufanisi.

Nadhani ungecheki na Dr. Agarwals wapo pale Morocco. Labda wameanza kufanya.

Ni delicate procedure ndo maana binafsi sidhani kama ninaweza mpa mtu jicho langu acheze nalo kiasi hiko.
 
Duh hadi spare battery, ndio naiona leo hii.

Itakuwa alikutana na majanga huko kabla. Watu wengine unakuta hana hata spare tyre wala wheel spanner.

Tunatofautiana sana.

Nilishapasukiwa tyre njiani baada ya kufunga spare tyre kabla sijafika sehemu naweza kupata nyingine nilikuwa sina raha kabisa maana najiona kabisa namiss kitu.
Ha ha ha ila gari za siku hizi haziji na spare tyre,wheel spanner wala jack. Zina run flat tyres ambazo inaweza kutembea bila upepo mpaka km80
 
karibu
unaelekea wapi?

Dereva wa ndege baada ya trip huwa wanalala pale Serena hotel au Hyatt Regency. Dereva ni mtu muhimu sana kabeba roho za watu na yake. So baada ya trip anatakiwa apate mahala pazuri sana na burudani nzuri kabisa za kuwek mwili wake sawa, akili kabla ya next trip.. ajali nyingi za madereva hutokana na madereva kuto kupata mapuzmiko sahihi hasa wanao tembea umbali mrefu.. hizo gharama ndogo sana Boss wangu
sijakataa ila mimi sina uwezo huo aisee
 
Duh hadi spare battery, ndio naiona leo hii.

Itakuwa alikutana na majanga huko kabla. Watu wengine unakuta hana hata spare tyre wala wheel spanner.

Tunatofautiana sana.

Nilishapasukiwa tyre njiani baada ya kufunga spare tyre kabla sijafika sehemu naweza kupata nyingine nilikuwa sina raha kabisa maana najiona kabisa namiss kitu.
Buti limejaa spare ukipiga tuta unazisikia kwa ndani.

Ni yule mtu akipata safari anaondoka saa hiyohiyo.

Hana haja ya kwenda service atafanya mbele ya safari.

Mnaweza mkawa sehemu kama mcity hivi mnapiga story, ukamwambia kuna deal twende mwanza, ana uwezo akaondoka na carina yake bila hata kwenda nyumbani kwake kuchukua hata nguo.

He's the most mobile guy i've ever seen.

Nikaona sababu ya yeye kubeba madude yote hayo.
 
Hivi Holy Man mwaka huu unaweza ukawa umetembea km ngapi?
Maana kama wewe, mimi pia lazima nisafiri kikazi...

Since January nimekula not less than 10000km highway
Paka sasa hivi kwa haraka haraka tokaea January ni zaidi ya 12,000km, kwababu ndani ya mwezi mmoja huwa natembea kati ya 2000km -5000km. Na kuna wakati trip moja tu huwa ninaenda zaidi ya +2000km non stop. Mfano kwa mwezi huu peke yake nimetembea 3,500km .. na leo usiku nakiamsha from Dsm to Tabora then mwanza..
 
Acha tu kuna gari simple tu ya 2013/14 Mercedes E class kama anayoitamani Holy Man ukiigusa unaona kabisa dunia mbili tofauti na gari za 2007 kushuka chini.
Gari yoyote kuanzia 2014 kwa level zetu Bongo ni nzuri sana acha hizo za 2019/20
😂😂😂 mkuu mda si mrefu naanzia kwenye ML350 japo itakuwa ya ofisi.. ila nitanyanyasa kiaina
 
Back
Top Bottom