Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Halafu sababu ya kuweka 30 hakuna. Pale hamna makazi na barabara hairuhusu watu kuvuka
 
Yaani nikiwa zone ile naenda 30kph halafu mtu ananipita mbio nikimkuta mbele anakula cheti najikuta natabasamu....😂😂😂

Baba Bataringaya weeweee..... bad of you...

Unatakiwa umtaarifu dereva mwenzio hata kwa signals jamani tuokoane barabarani.

Mie kuna kipindi posta waliweka mtindo wa hii barabara hairudi/one way inaingia tuu wakati mwezi mmoja nyuma ilikiwa inapitika njia zote.

Sasa ikawa Askari wanakaa mbele kama mita 300 kiasi huwezi geuza wakimbia. Aiseeh watu walikuwa wanakula fine halafu asubuhi mtu anawahi kazini.

Mie nilikiwa nikipita kwa miguu au gari mtu akitaka kukatiza ile njia inayotoka round about ya azam kwenda round about ya extelecoms namzuia utakamatwa na askari hiyo njia haiendi.

Wabishi walikuwa wananikumbuka mbeleni huko, waelewa waliepushwa na fine.

Emagine hakuna sign inayoonesha barabara haiingii halafu mbele unakamatwa.....🤔.
 
Sasa Kasie mimi na wengine tunaenda 30kph wewe na Crown yako unapita na 80kph unaona Sisi wote maboya? Halafu kama mnaenda opposite direction ni rahisi kumshtua na huwa nafanya sana ILA kama mnaenda direction moja kumshtua ni ngumu
 
Mapato yamepungua..🤭🤭

Kuna afande mmoja alinikamata sikusimama zebra crossing kupisha dada mmoja tuu avuke.

Gari ya nyuma yangu ilisimama, nashukuru afande alikuwa mwanaume....

Baada ya kuona nampigisha stori kwa wingi akaanza kunikagua, nikagundua fire extinguishers 🧯 yangu nilibadilishiwa maana afande akaniambia hii ina expire in no month wakati niliinunua January mwaka huu na ilikuwa na miaka 2 mbele.

Sijakumbuka ni wapi nilibadilishiwa fire extinguishers sababu huwa siikagui mara kwa mara, basi afande akaniachia nikaondoka nami nikamuachia tabasamu tuu 😊.

Triangle ziko poa.
 
Sasa Kasie mimi na wengine tunaenda 30kph wewe na Crown yako unapita na 80kph unaona Sisi wote maboya? Halafu kama mnaenda opposite direction ni rahisi kumshtua na huwa nafanya sana ILA kama mnaenda direction moja kumshtua ni ngumu

Nakuelewa Taibali madereva tumepishana, wengine washakipuliza, wengine wanawahi wakafumanie basi tafrani.

Itabidi nipange safari ya kwenda Kigamboni, kitambo sana sijapita huko.

Kuna kipindi nilikuwa natoka Central Police nanyoosha hadi mbagala kona ya kwenda Tuangoma nakata kushoto naanza kurudi hadi nafika Kigamboni aidha napita darajani au nateremka feri Kivukoni kisha naenda kula ice cream sno cream.

Kuna siku bange ilinikolea nikanyoosha goti hadi Vikindu nikapozi kama nusu saa kisha huyoo nikageuza hadi Kariakoo nikaenda jipoza na urojo 🤪.

Kasie Matata.
 
Hapo semi trailer za kubeba mbao huwa zinaingia porini zenyewe[emoji3]
Acha kabisa aise barabara mbaya sijapata kuona! Nilikuwaga nasikia tu kuwa Nyang'oro kuna kona mbaya kuliko hata Kitonga nikawa nabisha maana mimi nilikuwa naamini Kitonga ndiyo kuna kona mbaya ila jana ndiyo nikajionea mwenyewe!

Kweli kwa Nyang'oro Kitonga inasubiri aise! Maana Nyang'oro kuna kona mbaya halafu barabara zake nyembamba kuna sehemu mnapita hadi unajiuliza hivi hapa magari mawili yanapishana kweli hapa bora hata Kitonga kona zake zina space kidogo!

Halafu Kitonga huwa panachukua takriban dakika 10 kupamaliza ila Nyang'oro ni karibu dakika 20 hivi! Ila zaidi ya yote nimependa ile view ya Mtera Dam inavyoonekana kwa chini!
 
Kitonga jina kubwa tu ila hamna ishu.

Nyang'oro tamu aisee... nimeshuka na pikipiki mara mbili, nilifaidi sana.

This time nalala na zile kona na miguu minne mpaka nisikie tairi zikilalama
 
Chunya road! Kwenye zile kona zetu za mkoa!

Nimesikia jana kuna ajali imeua watano kwenye hii barabara ila sijajua ni wapi exactly! Leo matraffic wamejaa kila kona wamechachamaa wanataka level seats tu abiria yeyote anayezidi anashushwa njiani!

Sema hii barabara nayo ni kisanga kingine! Kona kali sana japo nayo ina breath-taking views kama zote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…