Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Acha kabisa aise barabara mbaya sijapata kuona! Nilikuwaga nasikia tu kuwa Nyang'oro kuna kona mbaya kuliko hata Kitonga nikawa nabisha maana mimi nilikuwa naamini Kitonga ndiyo kuna kona mbaya ila jana ndiyo nikajionea mwenyewe!

Kweli kwa Nyang'oro Kitonga inasubiri aise! Maana Nyang'oro kuna kona mbaya halafu barabara zake nyembamba kuna sehemu mnapita hadi unajiuliza hivi hapa magari mawili yanapishana kweli hapa bora hata Kitonga kona zake zina space kidogo!

Halafu Kitonga huwa panachukua takriban dakika 10 kupamaliza ila Nyang'oro ni karibu dakika 20 hivi! Ila zaidi ya yote nimependa ile view ya Mtera Dam inavyoonekana kwa chini!
Kitonga na Nyang'oro pamenyooka hivyo!

Siku pita Sumbawanga kwenda 'Bondeni' Muze ndio utajuwa Nyang'oro, Chunya Mby rd na Kitonga zote zimenyooka tu!

(Fuso unachekecha kukata kona! Gradient / nyuzi pembe za mwinamo ni almost 40 degree)

Hatari sana nja hiyo.
 
Tunasubiri trip zako za huko, hata siku ukienda racing tuwekee.

Hii corona imetumaliza mkuu
Nimemiss sana Silverstone ila wanafungua mwezi wa 8 kwa ajili ya F1 na bei zimekuwa juu sana

Gari zipo ila huwezi kujiachia kama huko
Hapa ipo Porsche GTS V8,
Benz C300, Range na Golf GTi chaguo lako
IMG_1164.jpg
 
Chunya road! Kwenye zile kona zetu za mkoa!

Nimesikia jana kuna ajali imeua watano kwenye hii barabara ila sijajua ni wapi exactly! Leo matraffic wamejaa kila kona wamechachamaa wanataka level seats tu abiria yeyote anayezidi anashushwa njiani!

Sema hii barabara nayo ni kisanga kingine! Kona kali sana japo nayo ina breath-taking views kama zote!View attachment 1810812View attachment 1810815
Beautiful scenery... enjoy mkuu
 
Back
Top Bottom