Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Polo ni Ka baby walker. Golf GTi ndio chuma kilichoumbwa kutulia.
Golf GTi inakuwa 2000cc turbo charged ambayo mwendo uko limited to 250kph stock, ukii tune unaweza kufuta kisahani 300kph.
Hapo mwamba ni Golf GTi maintanance hazitofautiani sana.

Thanks man.

Hapa Bongo kuna wataalaamu wa kufanya hizo tuning za magari?

-Kaveli-
 
Hii test yake nzuri mchana, usiku nitaiua gari ipo chini sana na sipendagi modification ya kunyanyua gari . Na mchana itabidi kujipanga sana kukabilina na trafic. Ila nilitest NZEGA to TBR kuna 127 km, nimetumia dk 30 .. kipande kizuri sana kilehakina tuta wala nini
Dah nakikumbukia kile kipande nasema ihiii...n
 
Kipande kitamu sana kile hakina Trafic no bams, na pia cha tbr to dodoma via manyoni patamu sana, shida kona nyingi
Dodoma to Tabora via Manyoni na Itigi sio? Aisee bonge la mkeka kona kitu gani tuko na sedans mkuu?

Mimi nilitumia 3 hours Nkuhungu (Dodoma) to Tabora, hizo ni 400km trip meter hiyo hapo, 127kmph average. Ile lami ni tamu MNO!

Nilianza mdogo mdogo Dom to Manyoni ila nilivoikamata ile lami ya kuitafuta Tabora nikaona usintanie, hii lami ni too good to go slow. Na hakuna magari unatembea 160kmph dkk 5 nzima hujapishana na gari. Na hapo ni usiku sikumwanga moto, sikupatii picha ulivyoipita mchana.

20210421_230732.jpg


Tabora Nzega pia ni burudani ila pafupi only 120km wakati Tabora to Manyoni ni around 250km.
 
Back
Top Bottom