Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ila ukiwa unaenda dodoma fupi ni ya manyoni, kuliko kupitia nzega.. mkeka ni mtaaamu sanaa.. nachopendea hakuna unafiki wa trafic kule.. unatembea tani yako
 
Pale opposite na kitete hospitali wanapika mchemsho wa kuku wa kienyeji unaitwa 'Abuja'.

Mzito kama roast, una hoho kibao unakuwa wa kijani kinyama. Ladha ya kipekee sana. Ndio kitu unique kuhusu Tabora, sijaona pengine.

Ila pisi za hii town ukiwa viwanja zina shobo hatari. Zinajirahisisha balaa. Kukufuata kukuomba uwanunulie bia sio ishu sana. Ukisalimia tu unaombwa bia.

View attachment 1815900
 
Naona kibao hicho. Yani barabara inapiga U turn. Hatari sana ukiingia kichwa kichwa
 
Naona kibao hicho. Yani barabara inapiga U turn. Hatari sana ukiingia kichwa kichwa
Acha tu mkuu barabara inapita juu ya milima na kuna sehemu kule juu lazima mkutane na yale mawingu yanayosababisha ukungu barabarani kwahiyo dereva inabidi uende mdogo mdogo tu hamna namna

Inasemekana ndiyo barabara kuu inayopita juu zaidi kuliko barabara zote Tanzania kutoka kwenye usawa wa bahari

Kona zake hata ile barabara ya Mombo-Soni-Lushoto sidhani kama inaona ndani kwa hii
 
RRONDO huu uzi hautufai wengi wetu humu. Unaweza kumuiga Holy Man ukaishia pabaya aiseee...masaa matatu dodoma to Tabora? Hahahah...bado nina hamu ya kuenjoy uchumi wa kati wa mama Samia...
Fanya kile unachopenda mkuu. Mfano mimi siogopi kufa na mambo na raha za dunia najuaga ni vitu vya kupita, kipindi tunapita lazima kukamua kile upendenacho😀😀. Tumezaliwa watupu na tutaondoka watupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…