Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kitonga na Nyang'oro pamenyooka hivyo!

Siku pita Sumbawanga kwenda 'Bondeni' Muze ndio utajuwa Nyang'oro, Chunya Mby rd na Kitonga zote zimenyooka tu!

(Fuso unachekecha kukata kona! Gradient / nyuzi pembe za mwinamo ni almost 40 degree)

Hatari sana nja hiyo.
Comrade naomba a b c za hiyo njia ya kudondokea bondeni kupitia Muze,
Je naweza kufika Kigoma kupitia hiyo njia ?Nina mpango wa kwenda hijja pande za huko ifikapo Augost
 
Comrade naomba a b c za hiyo njia ya kudondokea bondeni kupitia Muze,
Je naweza kufika Kigoma kupitia hiyo njia ?Nina mpango wa kwenda hijja pande za huko ifikapo Augost
Hapana huwezi kufika Kigoma moja kwa moja labda kwa kuongeza kilomita kadhaa za mzunguko na njia si rafiki sana labda upitie njia kuu ya Tunduma - Sumbawanga - Mpanda - Kigoma.

Ni njia ya kutoka barabara kuu Sumbawanga - Mpanda unachepukia somewhere NKUNDI / NTENDO kuelekea Ziwa Rukwa. Huko ziwani ama ukanda wa ziwani ndipo panaitwa BONDENI.

Bondeni kwa sababu kuna tofauti kubwa ya altitude na Sumbawanga mjini na Ziwani, Imagine Sumbawanga mjini nyuzi joto 17 za celcius ni kawaida tu lakini Bondeni una experience nyuzi joto hadi 35 centigrade (celcius)

Amazing fact:

Ukiwa nje ya mkoa wa Rukwa, Sumbawanga ndio Rukwa, lakini ukifika Sumbawanga mjini BONDENI ndiyo huutwa Rukwa! Actual ziwa Rukwa lipo huko bondeni.

Rejea picha nilizoweka (kwa hisani ya google) , Muse = Muze.

Kutokea Mbeya kwenda Kigoma kupitia Mkoa wa Rukwa kuna njia kadhaa zikiwemo:-

1. Mbeya - Chunya - Inyonga - Mpanda - Uvinza - Kigoma

2. Mbeya - Chunya - Innyonga - Majimoto - Mpanda - Uvinza - Kigoma

3. Mbeya - Mlowo (Songwe) - Muze - Ntendo - Namanyele - Mpanda - Uvinza - Kigoma

4. Mbeya - Mlowo (Songwe) - Muze - Majimoto - Kibaoni (Stalike) - Mpanda - Uvinza - Kigoma

5. Mbeya - Tunduma - Sumbawanga - Mpanda - Uvinza - Kigoma (hii ndiyo njia kuu.

Karibu utembelee kanda za huko, kuna mengi ya kujifunza, ikiwemo neno "ahsante" kama sehemu ya salamu.
_____
Asanteeeee!
IMG-20210620-WA0056.jpg
IMG-20210620-WA0057.jpg
IMG-20210620-WA0058.jpg
IMG-20210620-WA0059.jpg
IMG-20210620-WA0060.jpg
 
Back
Top Bottom