Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

New RR Beam ndio zinakuwaje mkuu? Usiku unaona mbele mita 500?!!

Ni bulb tu? Ama zinauzwa taa yote complete?

Ama New RR = New Rolls Royce ? 😁

Napenda sana lights kali usiku ili kuwajibu mafuso wenye akili mbovu, wale jamaa wanawasha full muda wote!!
Range rover mkuu. Taa zinamulika zaidi ya 500m mbele ila zikisense mwanga mwingine unakuja(gari) zinajipunguza zisimuumize anaekuaja.
Screenshot_20201222-073341.png
 
Hamna LC yenye 6 kwenye 200 series! Zote ni V8 tofauti inakuja kwenye Trim tu na fuel type.
GX ni mnyama sana, solid axle mkali wa all-terrain.

Engine ya Diesel ni 1VD-FTV ipo 200 series na kwenye LX 70 series mpya hizi. Engine ya Petrol ni 3UR-FE ama 3UZ hizi zipo kwenye 200 mpaka 100 series.
Hivi Prado TX zinatumia engine gani
 
Hamna LC yenye 6 kwenye 200 series! Zote ni V8 tofauti inakuja kwenye Trim tu na fuel type.
GX ni mnyama sana, solid axle mkali wa all-terrain.

Engine ya Diesel ni 1VD-FTV ipo 200 series na kwenye LX 70 series mpya hizi. Engine ya Petrol ni 3UR-FE ama 3UZ hizi zipo kwenye 200 mpaka 100 series.
Niliiona moja ya ubalozi wa Sweden V6 GX nilishangaa sana. Ni 4.0L 1GR-FE V6
 
Wakuu kwa anaetaka abiria nipo hapa, Dar-Arusha tarehe 24/12. Tutachangia kidogo mafuta, story za hapa na pale zitakuwa za kutosha. Ikitokea dharula ya kubadilisha tairi au yyt tutasaidiana ingawa mimi sy fundi.

Nichek chemba kwa mwenye uhitaji.
 
Naona tochi zimeanzia hapahapa mjini hivyo mnaotarajia kuanza trip muwe makini na kuwafaidisha hawa jamaa......asb hii nimewakuta njia ya Tegeta kati ya skanska na jkt ( pale kuna kibao cha 60) nafika huku kibada nimewakuta wengine wametega
Ilo eneo toka kitambo wanachapa tochii
 
mm yalishanikuta nimempa lift pisi kali kumpandisha mgombani toka Dar
Timing belt ikakata Makanya, mpaka kuja kugundua ni yenyewe saa nzima pisi niliyempa lift naye kapewa lift na majaamaa mpaka Same, ili wanitumie fundi wa injini kufungua cover waipate camshaft ili niondoke na sample au no. zake
Namkuta pisi keshalewa hatambui lolote eti kaniletee mizigo yangu asepe gari yangu mbovu.
km masaa 8 nikawa barabarani tena saa 2 usiku namkuta Same ni mzigo bora nikawa km wale madereva wa magari ya nyonya choo kweli wavumilivu, usiku nikamfikisha kwao, sitoi lift tena kwa hawa watu, hata pancha hainami?
Huwa sitoi lift, nakuwaga na redbul, mapakiti ya sigara na milaaa na maji yangu 😀😀😀.. nazima na mziki ili kupata utulivu.. au kama na mzuka nachapa country
 
Hizo za 5M ni brand new 200cc mkuu. Mhindi kazipatia hizi bike: Ziko njema mkuu, zinahimili mikiki. Hazifi hovyo, na zinatengenezeka. Bike yangu ina 52000km mileage. Major repair niliyofanya ni replacement ya valves at 47000km

Efficiency ni 30kmpl highway
Kwenye mafuta ipo vizuri Sana.
Mimi kwenye bike napenda iwe na mfumo wa valve 4 kwenye injini,sio kama hizi tulizoea zenye valve 2 (inlet 1, exhaust 1).

Napenda sound kubwa ya injini kuanzia 200cc na kuendelea.
 
Back
Top Bottom