Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Pole sana boss.

Huyo jamaa amekuokoa parefu sana.

Ungechukua namba mkale mbuzi siku ingine.
 
Mungu mkubwa kaka, watu wema bado wapo duniani!
 
Kwa mkasa huu, kwa crown, sipati picha ingekuwaje...

Pole sana mkuu
 
Pole sana ila bolt siku ingine toa moja kila tairi funga zinapokosekana, ikipungua moja sio issue.
 
Duh poleni, na hongera kwa jamaa kuweza kujali wengine.
 
Hiyo inatokea sana ..unaenda fanta service gari..mafundi wanafungua vituz hawarudishi vizuri ndo madhara yake..kama unaweza service fanta siku kadhaa kabla ya safari..siyo unafanya service hadi usiku ili kesho udamshe
Haraka mbaya sana. Juzi juzi hapa nimecheki coolant imepungua nikaongeza kidogo. Nikakurupuka nikaondoka kumbe sijafungua mfuniko uko juu ya engine top cover. Nimeendesha hadi petrol station almost 15km naweka mafuta mara taa nyekundu STOP CHECK COOLANT imewaka. Nikapaki pembeni kufungua bonnet expansion tank iko wazi kifuniko kiko juu ya engine!
Ikabidi ninunue maji ya Kilimanjaro niongeze,zilienda Lita 3 ila hakukuwa na madhara mengine yoyote.
 
Ni noma..unamwambia fundi acheki breakpads anacheki..kurudishia tairi anawapa vijana...haraka haraka nati wanaegesha tu..wewe kesho unanza ligi road lazima yakukute..au wanapuliza air filter alaf hawarudishi vzuri u unategemea nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…