Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Madereva wengi wana papara sana halafu sio wazuri kujaji umbali,mwendo wake na mwendo wa anaekuja.
Kweli kabisa mie gari la manual kama hilo li TD42 siwezi kuhangaika ku overtake wakati naona mbele hapako clear!

Gari yangu tu lazma nibust overdrive ikiitika ndio natoka mwendo wa ngiri yani rpm inaweza ikavuta mpaka 7 ikiachia mwendo wa kupepea tu dkk 0 nimerudi site! Sitanuagi kindezi bila kuona mbele
 
Mtu unaenda sehemu km500+ unashindwa kusubiri dakika 2-5 upate sehemu nzuri ya kupita?!
 
Mtu unaenda sehemu km500+ unashindwa kusubiri dakika 2-5 upate sehemu nzuri ya kupita?!
Watu wanajiaminigi sana yani unakuta hapo kilichowacost jamaa papara zao tu na kutokupiga hesabu za haraka. Yani ninachohisi ni kuwa inawezekana wote walitanua hawa!

Ractis alitanua akakata magari akajiwahi kurudi mbele ya basi kufika upande wake nae anaona Nissan imeiva inakuja usoni ikabidi aminye breaks ndio akajaa mbele ya basi na jamaa wa Nissan ikabidi aforce kuhama lorry likawa lishafika akabararuliwa na tyre za lorry na kurushwa juu ya roof ya ractis!
 
Uko sawa kabisa wife material, sema jamii zetu hizi nzito sana mbona mm nikiwahi home napika tu na wife akija anakula maisha yanaenda wanangu nawaosha tu.
 
Ni kweli uliye naye usimuache aende
 
Ndio maana huwa sipendi bus au lorry linikalie karibu mbele au nyuma
Nakuwa na amani kukiwa hamna gari mbele wala nyuma yangu. Naachaga following distance kubwa sana. Jitoe akili uniovateki uingie kwenye hiyo safe area yangu.... nikiwa na kichaa na pakiwa safe hutaamini ninavyoiziba chap unahangaika kurudi au kutafuta mnyonge mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…