Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Usijali "I know my car"..
Na ndio maana sijaita la mwingine..

"Be Humble"
 
yaani unabidi uwe mpole hawa jamaa nao wanajifanya vichwa ngumu hawaelewi
mwanzo walikuwa wakikuta Faini imefika 60,000/ au faini 2 wanakushauri ulipe kwanza, lkn kwa sasa wanakung'uta tu jamaa yangu wamemtundika mfululizo ndani ya siku moja
Pole yake aisee...huyo siyo dereva...faini zote hizo kwa siku..?
 
Wazee wa tochi wanakaa sana hizi sehemu. Tena wanakaa zile zinazochosha wanajua hapa uvumilivu utatushinda.
Mie ndiyo maana naipenda sana radarbot. Sema inafaa mkiwa mnasafiri zaidi ya mmoja mwingine anakuwa anamsaidia dereva kuangalia zile cams ziko maeneo gani na hao wazee wa tochi wako maeneo gani.
 
Hakuna basi inayoweza kushindana na gari ndogo(sizungumzii Passo au IST). Btw haya mabasi hayana ving'amuzi.
kweli kuna haya mabasi ya kati, km FUSO injini nyuma kina ROSA nina wasiwasi vidhibiti mwendo wanachomoa au hawaweki
nilishaumana nalo kwenye speed 110km/h simkuti mpaka nilipovuka 120-130km/h barabara ya Makuyuni kwenda Babati hiz basi za Hanang na huko Serengeti si mchezo
 
Nilipiga honi lakini haikusaidia
Hawa vijana wa Malori makubwa wakati mwingine wanapewa Malori mabovu hivyo anakuarifu usikae mbele yake mita chache km anakujali.
Niliovertake mlori upo tupu kati ya Magubike na Dumila wakati kwa mbele kuna jingine linakuja umbali km wa kiwanja cha mpira ile hamadi nimemaliza kukipita kichwa kumbe mbele barabara ni tuta la viazi, sasa uyapande ili ajae mbele apite site yake,
kile kitendo nikiwa gia ya chini kikapunguza mwendo kumbe mlori wa nyuma mteremko breki zimefaeli mwenzangu ni honi na kupangua magear
nilikanyaga na kuhamisha gear mpaka Dumila TRA chooni nikajisaidia napumua
jamaa kafika akaniambia usirudie kuOvertake halafu ukarudi ghafla au ukapunguza mwendo mm breki manati navutaa sana ndio zikubali ningekuingiza uvunguni na familia yako.
Kama kuna dereva anajua huo mshtuko wake ni tumbo la kuendesha kwenye kiti
 
[emoji16][emoji16]pole sana mkuu....naijua vizuri hali iliyokutokea....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…