Hawa vijana wa Malori makubwa wakati mwingine wanapewa Malori mabovu hivyo anakuarifu usikae mbele yake mita chache km anakujali.
Niliovertake mlori upo tupu kati ya Magubike na Dumila wakati kwa mbele kuna jingine linakuja umbali km wa kiwanja cha mpira ile hamadi nimemaliza kukipita kichwa kumbe mbele barabara ni tuta la viazi, sasa uyapande ili ajae mbele apite site yake,
kile kitendo nikiwa gia ya chini kikapunguza mwendo kumbe mlori wa nyuma mteremko breki zimefaeli mwenzangu ni honi na kupangua magear
nilikanyaga na kuhamisha gear mpaka Dumila TRA chooni nikajisaidia napumua
jamaa kafika akaniambia usirudie kuOvertake halafu ukarudi ghafla au ukapunguza mwendo mm breki manati navutaa sana ndio zikubali ningekuingiza uvunguni na familia yako.
Kama kuna dereva anajua huo mshtuko wake ni tumbo la kuendesha kwenye kiti