Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Yaani kila sehemu hiyo Dar pana/paliwahi kuwa na maeneo ya uswahilini
Obay na Masaki hapajawi kuwa na hakuna uswazi. Aliokwambia paliwahi kuwa na uswazi akwambie wapi. Usikute mnazungumzia Msasani maandazi road na bonde la mpunga. Maeneo ya mkoloni hayo wamejenga miaka hio sehemu tupu zilikuwa na mashamba ya mkonge.
 
Nashukuru Sana mkuu.

Nimeweka utani sijalalamika.

Hayo mengine ya Kua deal au sio deal nafunika kombe....

Muhimu uhai na afya njema. Mungu awajalie afya njema.
Usiwaze mkuu. Kuna jamaa mmoja humu anajiitaga nani sijui yeye kwenye zile nyuzi zinazohusu sijui kutaja member unayemkubali au kumtakia member unayemkubali heri ya sikukuu fulani huwa analalamika kuwa hajawahi kutajwa.

Na kuna siku alishawahi hadi kutishia kuondoka jf mazima kisa anaona hapendwi na watu hivyo hana maana. Nikasema duuh hii ishu unaweza kuta tunaichukulia poa kumbe kwa wengine ni serious hadi wanawaza mambo ambayo hayapo.
 
Sasa uneishi huko halafu hujui kuwa ni mitaa au nini [emoji15][emoji15]
Mie najuaga ni mitaa pamoja na hizo alizotaja extrovert. Sasa alivosema ni majimbo ndiyo kanichanganya, kuwa usikute mi miaka yote najuaga ni mitaa kumbe kitambo yashabadilishwa yamekuwa majimbo, maana hii nchi kila mwaka vijiji, mitaa, kata, majimbo, miji, majiji, wilaya na manispaa mpya zinazaliwa.
 
Ndio mchezo wangu huo. Yani taa zikiwaka kijani na hamna boda boda around ninachomoka vibaya mno
Achaneni na hio njia! Kuna siku natoka Mwenge nimeiachia taa zote kijani kufika hapa ilipokuwa Halotel zamani kuna jamaa akaingia na Crown niko 100+ nilipiga breki moja nikaswerve kushoto nilimkosa kama cm mbili nikajikuta nimefunga barabara zote mbili. Hizi barabara za mjini sio kabisa kuna wehu zile taa kwao hazina maana.
 
Alikuwa anawahi nyekundu ya upande wake sio? Taa za ile barabara ya mwenye zinakuwaga kijani muda mrefu mno, unapoikaribia intersection kuna kila sababu ya kupunguza mwendo kwanza maana watu uvumilivu unawashinda wanazivukaga.
 
Hata sijui alikuwa anafikiria nini, ndo maana nasema hizi taa usiziamini kuna mwenzio anaosha tu.
 
Hapo unaweza sali salamu maria kwa speed ya mwanga.

Ila kusafiri usiku ni changamoto sana mkuu.

Unaweza kutana na hatari 50M toka ulipo, hata ukiwa 100kph, maamuzi ya ghafla hayasaidii sana. Mind you usiku ndo wanatembea wabovu wote wasioruhusiwa kutembea mchana.

Pole sana.
 
Obay na Masaki hapajawi kuwa na hakuna uswazi. Aliokwambia paliwahi kuwa na uswazi akwambie wapi. Usikute mnazungumzia Msasani maandazi road na bonde la mpunga. Maeneo ya mkoloni hayo wamejenga miaka hio sehemu tupu zilikuwa na mashamba ya mkonge.
Sehemu wanakaa mabalozi wote ukute uswahili.?

Labda wale waswahili wanaoendaga Coco Beach kula mihogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…