Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Hatari [emoji1][emoji1]
 
Hahahahahha eti alichochewa Ngumi
 
Mimi siku hzi nna tatizo la kuendesha usiku town, zile taa za kumulikwa tukiwa tunapishana zinanizingua sana, kiasi siwezi kutembea zaidi ya 50 kph. Nakuwa na tension sana...ukizingatia gari yangu Taa zake kidogo zilishika ukungu kwa hyo sio kali sana kumulika barabara..

Hapa nisafishe taa au nikapime Macho? Kuna Raia wanakupiga full mpaka machozi yanatoka.
 
Vyote viwili 😛😛😛...sababu ya kukwepa kusafiri usiku ni hii,nahisi uwezo wangu wa kuona usiku umepungua kwa kiasi kikubwa.
 
Mm huwa nazima zangu Kwa sekunde chache alafu nawasha full direct nikiona mbishi nakuletea goma huko huko.

Kuna madereva wanatembelea full nyakati zote. Kwa madaladala ninq chojua ni switch za taa zinakua zimesha kufa ukiwasha taa inawaka full moja Kwa moja.

Wengine macho yamepungua nguvu so inabidi awashe full Tu.

Tafuta miwani ya kuendeshea usiku, ongeza bulb zenye Wats kubwa na kapime macho.
 
MWingine unakuta inawaka moja,akiweka full ndio anapata mwanga kidogo. Halafu unakuta ni bulb tu ya kubadilisha.
 
Huwa nabaki kusema tuta hili kaweka mtu asie na gari @##__&&&& zake! Gari ikikwaruza hadi utumbo unageuka! Hadi tumejifunza trick ya kupanda kiupandeupande. ILA Dar-Arusha, Dar-Dom sijapita tuta lolote gari ikagusa chini. Kilikuwepo kituta kimoja kabla ya kuingia Korogwe ILA wamekitoa kilikuwa kama Gogo la mnazi!
 
Hao wanaotembelea full nyakati zote utafikiri wanawinda huwa nashindwa kuwaelewa. Huwezi kuwaletea shida wenzio wengi kisa wewe mtu mmoja kwa tatizo ambalo unaweza kulitatua.
 
Kama ilikuwa vanguard nyeupe tulikuwa ni sisi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…