Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Sasa juzi jamaa alikuwa hana mtu wa kushindana nae ndio shida 😂😂😂
 
😂😂😂😂😂😂 ningekucheka sana, kwa Crown inavyochomoka vile sioni kokote kwa mtu mwenye 15Ohp kukusumbua ikiwa utaamua kumyoosha. Subaru EJ2O ina nguvu ila sio kama inavyokuwa hyped. Hata mtu mwenye 1.8L ya Toyota kama 2ZZ-GE anaweza kumfua Forester vizuri tu. 2ZZ inafua 18OHp.

Huwa jioni nina tendency ya kutembea njia ya Makumbusho hadi Victoria and back. Mambo ninayoona kwenye Crown acha watu wazinunue tu.
 
Nahisi dunia nzima magari yanasajiliwa kwa manispaa na majiji. Na ukihama unaweza sajili tena unapohamia ni kukeep track. Ila tz ndio hivyo TRA ni kila kitu
Upo right kabisa mkuu, nani na wapi tulikosea kama nchi?,cha kushangaza driving licenses nazo zitoke TRA?hii si sawa,traffic department ndio ihusike na driving licenses, wao ndio ilitakiwa wasimamie utaratibu wa kutoa hizi licenses (mtihani wa maandishi na practical one),tunahitaji systems imara na itakayounganisha nchi nzima,TRA washughulike na ukusanyaji wa kodi kubwa, kodi zingine ziachiwe municipalities/metros kukusanya henceforth kujipatia mapato
 
Fair kabisa tena huo ni mwendo wa kawaida kabisa,Dar to Moshi ni +500kms,wastani wa 120km/h inatakiwa hiyo safari iwe imeisha, Windhoek to Katima mpakani na Botswana na Zambia ni kama 1400kms,watu wanafukia umbali huu kwa 9 to 10 hrs, na huu ni mwendo wa kawaida kabisa
 
Hii unapiga 5 hours bila kukamia

Sent from my MAR-LX1A using JamiiForums mobile app
 
Kwa coaster ina utata...sijui huyo jamaa alikuwa anaendeshaje especially vile vipande vyenya matuta, maana mitaa ya Iringa barabara imewekwa tutaz za kutosha
Tuta ndani ya freeway sijui engineers wetu wanafeli wapi, halafu inaonekana hawa engineers wote hapa nchini thesis zao ni kuhusu matuta kwenye freeways, mituta ya mikumi national park ni upuuzi mtupu, mkeka wa iyovi tutas mpaka porini!,down ya mafinga Ile tuta zile zinaua suspension za gari ni craze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…