Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

11M+ what a joke? Tujiandae kupanda punda for real! TRA wakishaona gari zinaagizwa kwa wingi ndipo changamoto inapoanzia.My worst fear ni pale watakapoanza kudeal na biashara ya spare parts kwa kuitoza kodi kubwa.
Uzuri Wabongo sio rigid,watatafuta gari ingine yenye unafuu watakomaa nayo. Wakipandisha wanahamia ingine.
 
TRA wanachokitafuta watakipata soon,
Wao badala waje na njia bora za kuleta ahueni ya kodi ili watu walipe kwa wingi, wao wanakomaa na kuongeza kodi .

Mara sijui kodi ya kitanda kwa watalii....watalii wakienda Kenya TRA mtachukia..?

Kodi za magari wanapandisha...wengi watauziana magari ya mikononi..

Tutafufua zile gari za zamani tuziweke barabarani.
 
Na mimi naona dalili za madalali kupiga pesa kuliko hata TRA,ni mwendo wa kuuziana used za kibongo bongo kwa sana.
 
Hawa jamaa wanaweza anza kuongeza tozo la transfer ya kuuziana magari mkononi wakiona watu hawanunui sana japan 😁 😁 😁 .Kama wanachaji vitanda hata siwaamini
😃😃😃 sasa hapo inabidi kurudi enzi za yesu(kutumia Punda) au kama vipi watu watakua hawabadili majina kwny kadi ya gari ila siku kikinuka itafahamika mbele kwa mbele tu.
 
Hakuna jambo hatarishi kama kununua gari lenye Cc nyingi awamu hii,manake linaweza kukugeuza wakala wa mapato ya serikali hasa kwenye kodi ya mafuta na bado unakuwa huna uhakika kama hiyo tozo itaongezwa au lah! ni very risk project kwa haya mazingira ya sasa-Nilikuwa nataka ninunue mojawapo ya gari lenye 6 cylinder ila for now it's a big no na wala sishauri mtu.Ni swala la mda tu mtaanza kuona watu wanapak magari nyumbani bila kupenda
 
Hawa jamaa kuna kitu kidogo sana wanashindwa kuelewa,Wakitujengea mazingira wezeshi ya kuagiza na kumiliki magari na watanzania tulio wengi tukaweza kuyamudu na kuyatumia katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku,serikali itaweza kupata mapato mengi inayokusanya kupitia tozo ya kwenye mafuta achilia mambo mengi.Sasa wakieweka matozo makubwa na kila mtu akaamua kupark gari nyumbani au kutonunua si ni hasara kwao?
 
Wanamkamua ng'ombe sana mpk atatoa damu na mwishowe atakufa,hata yale maziwa kidogo hawatayapata.
 
Mafuta, Vipuri, Services, Car Wash

Gari moja lina multiplier effect kubwa kwenye uchumi.

Mapaka wale vijana wa car wash, mafundi n.k wanafaidika kukiwa na magari mengi.

Ila wanavyobana hivi. Hata hizo fuel stations zitafungwa.

Na polisi wao watakosa faini za barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…