Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Hiki hutokeaga kwangu hasa nikichanganya sheli. Mara nyingi huwa naweka Total nikiwa mjini ila siku za safari huwa naweka wese la Lake oil full tank.Duh leo nimetenda dhambi roho imeniuma sana. Nilikuwa na gari sijaizoe. Taa ya mafuta imewaka range inanionesha nina km20 tu. Nikaamua niweke mafuta ya kunifikisha home tu nikaweka 10,000 nilijua itaongeza range hadi km60 hivi. Baada ya kuweka mshale haukusogea wala range haikubadilika. Nikaenda ninapoenda range inashuka.
Kurudi nikapita njia ile ile range iko 14, nikapita pale kituo cha mafuta nikamwambia Yule dada nimeweka mafuta hapa kwako lakini gauge haikupanda wala kuonesha kuna mafuta yameingia, umeniibia! Dada Yule akasema sijakuibia nimekuwekea hela ulionipa nikamwambia haiwezekani kusiwe na mabadiliko kwenye gauge, ikabidi niende kituo kingine nikaweka 10, aisee gauge ikakurupuka ikapanda sana na range ikaja kwenye 110km. Hapo nikajua ni kweli aliweka mafuta nimemsingizia tu. Nimejisikia vibaya sana.
Sasa mara chache hutokea nataka niweke mafuta katika zone ambayo hamna total. Huwa sipendi kutembelea gari inayowaka taa ya mafuta hivyo nalazimika kuweka mafuta kwenye visheli uchwara kama Oilcom, Meru n.k Hapo ndio mziki sasa.
Gari yangu hunionyesha mabadiliko kwenye gauge after 1.5km distance maana nina katabia ka ku reset trip meter kila nikitoka sheli. Ikitokea haijafanya hivyo huwa nafadhaika sana na kuisi nimeibiwa hela bure kumbe wala inakuwa sio kweli.