Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

kwa Chalinze - Moro nakubali km una mashine nzuri dk 75 hazifiki
kuna vibonde na miinuko hasa kule pori toka Mdaula mpaka Mikese pale hata 140-180km/h unakanyaga.
Hapa tusaidiane mafundi, dereva anaposema kakanyaka mafuta hadi speed 180km/h ikasikia injini inazima au kuburst ukweli unatokea wapi?
Mimi niliunguza alternator nikajua ni speed niliyotumia kwani nilikimbia zaidi ya saa nzima nikiwa 120 -140km/h
nilipoenda dukani nikamwambie aniuzia Alternatoe ingine kwani speed niliyotumia sio mchezo, yeye akanicheka akaniambia mzunguko wa injini upo palepale na belt zake ni hii ni kutokona na RPM kinachokimbiza gari ni gearbox na hasa Top gear
unaweza kukuta upo speed 200km/h na RPM ipo 7 na ndio mzunguko wa alternator
ina uunaweza kuwa speed ya 40 km/h RPM 10 (nina maana ya juu kabisa)

nipo tutani nasubiri majibu yenu
Kama engine yako iko vizuri unawezea tembea siku nzima kwa spidi yoyote. Ukiangalia dashboard kwenye ile gauge ya RPM utaona kuna red zone kule mwishoni. Gari za petrol nyingi red zone inaanzia kwenye 6 na za diesel ni kwenye 4.5. Hii red zone ndio sio ya kukaa mda mrefu, unaistress engine.

As long as unatembea chini ya red zone hata kama upo 180km/h engine yako haitakiwi kuchemsha wala kuingia tatizo lolote. Imeumbwa ili itembee.
 
0C571F4B-7B2B-437F-8F98-DB9A88B2FF63.jpeg

Bampa to bampa 🤨

Baridi pia inaleta hasira, ole wake mtu anichomekee 😅.
 
Hii ndio Overtake inayotakiwa kwa gari zaidi ya 3 mpaka 7 au zaidi za aina tofauti km malori na ndogo.
Unaweza vta mafuta ili kuunganisha ukashtuka mwenzako wa 3 mbele huko naye anachomoka na uwezo hanainabidi ukajifiche kushoto, usubiri tena, ni vizuri kujificha nyuma uki time mmoja mmoja na sio kwenye kona
View attachment 1698881
Inategemea na chombo ulicho nacho, barabara ilivyo pia. Kama imenyooka na umeisha ona zaidi ya 2 km.. nyeupe haina kitu, hata kama 10.. unazikusanya, ila kama huoni zaidi ya 1 km.. na road ina kona. Ni vyema uwe mpole
 
Juzi alfajiri kijana akitokea Club anakowahi hata sipajui kigizagiza kayumba na kaja kunivaa upande wa site yangu na kunigoganga side ya kushoto, anatoka ndani ya gari ananiomba msamaha eti aliona anatoka nje ya barabara angepinduka akaona bora arudi barabarani ndio mm nikawa breki yake.
Kupeleleza ni Marioo na gari ni ya mwanamke, yeye alichomoka kwenda kulewa, Tukajadiliana na Traffic ikaamuliwa akalitengeneze na mm nizuie hilo lake (la mwanamke wake) mpaka langu lipone.
Ni kweli barabarani ni Mungu tu anasaidia, unaweza fuata Sheria zote bado mlevi akakufuata akijua mnapishana kumbe anakuua
Brooo ndio umeamua uje unisimange na humu Jf daaah 🥲🥲🥲
 
Sasa umesimama kwenye traffic lights wa nyuma mlevi utafanyaje?
Hapo inakuwa haina namna , atakubutua tu. Ndio maana yangu ya kusema ingawa haiwezi kuwa 100%. Vyanzo vya ajari vingi ila tunajaribu kuvi punguza tu kadri tuwezavyo. Ni sawa mie leo almanusa Scania inipasue, ila nikawahi kutoka barabarani, nahisi lili fail, nikaliona hilo .. nyuma yangu..
 
Brooo ndio umeamua uje unisimange na humu Jf daaah 🥲🥲🥲
Unapo endesha gari, unatakiwa uwe dereva wa gari tatu. Ya nyuma yako, pembeni yako na mbele yako. Japo sio 100%. Mengine mkono wa shetani unaweza kusudia kukuharibia siku
Tatizo pombe Mkuu ulikuwa umebwiya haswa, mpaka suruali haitamaniki ina maana wakati ajali ianakufika ulifikiri upo choo kikubwa ukaona uje upaki kwangu km kigingi wakati breki ungekanyaga tu
safari nyingine usinywe ukaendesha gari, ukiwa mzima unaonesha utu hasa Mkuu
😀 🤣😂
 
Jana nlikua Safari na BM Coach(VIP's & Private Seaters), Dereva ana kovu kwenye paji la uso mixer Upara na Pete ya Ndoa ya gold. Plate namba ni DPF(Namba naihifadhi). Yaani huwezi amini kila nikibook BM nakutana na huyu Dereva. Sasa nnachotaka kusema hapa ni kwamba kuna watu tukubali wana vipaji vya kuendesha magari na wengine tunaiga au kulazimisha fani.

Huyu Mwamba ni Shida. Kwanza sijawahi kumuona kakamatwa alafu safari zake zote iwe route ya Dodoma, Moro au Moshi~Arusha ni mwendo wa speed 40 to 48km/h. Anazingatia Vigezo na Masharti ile ile na anatembelea Manual. Salute kwake.

Haijalishi mtafika saa ngapi lakini mwamba anakazia humomhumo na anajali muda huyo Khataree, kuna Njemba iliomba kushuka kuchimba dawa sehemu isiyo rasmi, dereva akampa Chupa kubwa lile la Lita 2 akamwambia ajiongeze. Nikazidi kumuelewa.

Aafu, kuna Bi Mkubwa juzi kati alivurugwa akapayuka anataka nyimbo za Dini kwenye gari eti hapendi kuona viuno vya wadada wa BongoFlavour wakiwa nusu Uchi Mwamba akamute Sauti kisha tukatembea kama masaa 4 hivi bila Volume kisha akaichia ilivyofika kwenye sinema. Bi Mkubwa Kimyaaa!!!

Kwa mawazo yangu ni Mkali wa hizi kazi na uzoefu unachangia.
 
Back
Top Bottom