Duh POLISI hawakimbiwi hasa kwa madereva wa kila siku
Niliwakimbia Traffic Singida kuelekea Manyoni, kuna kona moja akatokeza porini jamaa ana camera akanipiga mkono kumbe bado nipo Mji wa Singida, nikampuuza. akapiga simu Ikungi ni kawilaya kadogo kapo mbele, duh nikaona malori ya mbele yangu yamesimamishwa na mm pia, wakataka leseni yangu nikawapa
Wakaniambia shuka usikilize mashtaka, eti nirudi Singida nimemkimbia Traffic, nilibisha wakaniambia park hapo Kituoni mpaka utakapoenda Mahakamani.
Nipo na familia na cent ndio imebaki 19,000/ walinipukutisha zote
sirudii kuwakimbia hawa jamaa, wanaambiana kwa simu za kawaida na wala hawakufukuzi, anaweza kukuambia washa wiper, kumbe anakuvuta