Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mimi jana nilipiga 1300km in 26 hours. Niligeuza the same day jioni kutoka Arusha nikarudi Dar.

Fatigue ingeniua.

Niliona reaction time yangu imekuwa mbaya mno, ikabidi niache kumwaga moto nikawa naifuata gari nyingine nyuma namtumia kama guide wa kuniangaliza mbele.

Kufika mombo nikakunjua kiti cha abiria nikajilaza, nkashtuka lisaa limoja na nusu baadae nikiwa fresh. Ikawa ni kulala na kona za korogwe tu - sedans zina raha yake kwenye curves.

Fatigue is real. Usingizi hauna baunsa.
Duh si mchezo!
 
Mwenye heshima yake mpe

20210318_094536.jpg
 
Bike ina starehe yake unique sana ukiwa unasafiri mchana. Ulishawahi kujaribu Iron Butt Association challenge? Kutembea na pikipiki 1000km ndani ya masaa 24 consecutive?

Kweli inahitaji Iron butt. Kalio linaumia kishenzi
Hapana sio member wa Iron Butt, halafu hapa nilipo hakuna mtu mwenye mashine kama yangu kwa hiyo uwa nikaamua kuitembeza,natembea pekee yangu. Umbali mrefu niliowahi kusafiri ilikuwa Dar - Mwanza, kama mara tatu hivi. Kama hakuna mvua na upepo mkali nikiondoka asubuhi kabla jua halijazama nakuwa nimefika upande wa pili
 
Back
Top Bottom