Pole
Saint Anne Mungu akitie nguvu usipoteze imani, moyo huuma, huzuni hujaa ila wakati ni dawa maana akili husahau.... na muda ukienda hata ukikumbuka uchungu na huzuni haviwi kwa kipimo kile.
Haya ndo maajabu ya Mungu, ukimtegemea na kumuamini hakuachi. Roho, nafsi, utashi na akili ukijumlisha na moyo ndo utu na ndo mwanadamu.....
Linda sana moyo wako, maana ndiko zitokako chemchem za uzima.
Nawaombea mmalize shughuli za mazishi salama kwa amani na upendo. Pole nyingi zifikishe kwa familia pia.
Pokea kumbato la faraja kwa namna ya rohoni kutoka kwa bibi Kasinde.
Pole sana Anne.