Alubati
JF-Expert Member
- May 29, 2016
- 6,535
- 14,840
Hujapiga hata picha hiyo view ya mtera,si unajua ukifatilia huu uzi na unajiona kama upo safarini vile..Acha kabisa aise barabara mbaya sijapata kuona! Nilikuwaga nasikia tu kuwa Nyang'oro kuna kona mbaya kuliko hata Kitonga nikawa nabisha maana mimi nilikuwa naamini Kitonga ndiyo kuna kona mbaya ila jana ndiyo nikajionea mwenyewe!
Kweli kwa Nyang'oro Kitonga inasubiri aise! Maana Nyang'oro kuna kona mbaya halafu barabara zake nyembamba kuna sehemu mnapita hadi unajiuliza hivi hapa magari mawili yanapishana kweli hapa bora hata Kitonga kona zake zina space kidogo!
Halafu Kitonga huwa panachukua takriban dakika 10 kupamaliza ila Nyang'oro ni karibu dakika 20 hivi! Ila zaidi ya yote nimependa ile view ya Mtera Dam inavyoonekana kwa chini!