Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kweli mkuu sijui umetumia gari gani ila mfano kama LC V8 zina uwezo wa kutumia 4hrs tu from Dar to Dom ndiyo maana hata viongozi wakubwa wanaoendeshwa kwa hizi gari wana uwezo wa kuja Dar kila ijumaa jioni kuspend weekend nzima na kurudi Dom kila jumatatu asubuhi kuendelea na kazi! Wenyewe wanakuambia Dom hakujachangamka hivyo hapafai kula bata ndiyo maana wanatamani kurudi Dar!

Kuna siku Mwendazake alikuwa Mbeya na msafara wake imagine from Tukuyu to Mbeya mjini kwa gari za kawaida ni mwendo wa karibu lisaa na nusu lakini LC V8 za msafara wa Rais zilitumia nusu saa tu from Tukuyu to Mbeya! Yaani Mbeya mjini gari zote ambazo zilikuwa kwenye barabara ambayo msafara wa Rais ulitakiwa upite zilisimamishwa Mwendazake akiwa Tukuyu na baada ya nusu saa msafara ukawa umeshateremka Mbeya mjini!

Kwa sie SUV enthusiasts tunaona hapa kweli mjapan alitulia! Ndiyo maana binafsi kwa SUVs za mjep nazielewaga sana LC VXR V8 na NP Y62 V8 hizi gari huwa naziheshimu sana ni moto wa kuotea mbali!
Safi sana mchumba,,, hii ndio mambo ya maana sasa nitaku add kwenye group la team cruiser 😅😅😅!

Umeichambua vyema V8 ila sasa kwa toleo waliotoa sasa la 410HP V6 kitakachotokea sasa Dom watakuwa wanatumia 3 hours! Ni V6 iliochangamshwa na turbos Toyota hana mchezo yani hata ile Y62 inakalishwa!
 
Mwenzio yalinikuta. Nimetoka mbali vizuri na alphad ile naianza kibaha nikawa nahisi usingizi ila nakazaa macho nasema nimesha fika hapa ntalala home. Kufika kibamba nikapiga mapipa yale ya ujenzi wa barabara kumbe nilisha sinziaaaa kitamboo. Mguu wa kushoto mbele na bumper vili ishia pale. Confortability ya gari huongeza raha ya kausingizi.
Ukiona hio hali ni muhimu kujiwahi na energy drink + water! Dilute energy drink na maji kunywa glass nzima ya fasta usingizi ungekata
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Eeeh!!

Ilikuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitoboa tank wakati narudi 😅 nikaua bush kama zote basi gari chini huko inapiga vigeregere kama hiace mbwa kachoka zile! Nafika mbalizi nikashusha Tank na kuziba hizo Tire moja ikakata uzi nikafunga jingine jipya!

Ile njia niliambiwa shortcut ila ilikuwa wrong cut bora ningezungukia chunya mpaka Saza
 
My Favorite roads 2021 kama unapenda kunyoosha goti!
1. Manyoni - Tabora (Via Itigi hatari sana but usipate breakdown hakunaga msaada ile njia[emoji1787]
2. Arusha-Longido
3. Arusha - Manyara, na Kondoa- Dom
4. Biharamulo - Muleba
5. Makambako - Igawa (sema mchana kuna tochi kali sana)

My Best Sceneries

1. Moro - Iringa
2. Mbeya - Kyela (Nature ya hapa ni balaa)
3. Arusha-Namanga (Landscapes, vilima, wanyama)
4. Muleba - Chato (driving along Lake Victoria)
5. Himo-Marangu, Kilema, Rombo (hizi njia ukipata muda pita tu hata bila sababu kunavutia sana sana)
6. Mombo- Lushoto
7. Mbeya- Chunya
8. Mara-Serengeti- Ngorongoro Arusha Kama una gari ya juu don’t miss this

Zingine muongezee wazee
3.Arusha- Manyara,Babati hio ni kama Autobahn kibongo bongo 😂😂😂! Kimsingi highway zote zilitakiwa ziwe namna ile sio mituta kila mahali!!!
 
Back
Top Bottom