Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wale wanaotumia Morogoro road mjipange na tochi kwenye hii super high way yetu. Nimekutana na jamaa wa tochi hapo baada ya St. Jospeh kabla ya Mbezi.
Hapo wataokotwa wengie sana.. maana watu wanajiachia vibaya.. na lengo lao kukusanya pesa hapo.. siku hizi nimeona wanategea maeneo ambayo ni lazima goti likunjuke.. uzuru hizi siku za karibuni wananibutua tochi ila mwendo wanao nikuta nao huwa wanachoka wenyewe.. nalipa 30, ile kiroho safi
Mi nimetoka saa 11 mjini, wazee wameingia barabarani nishafika mbali. Sema asubuhi niliwaachia ya kubrash viatu wazee wanaotega chalinze pale kwenye vichaka, kuovertake sehemu yenye mstari usiokatika.


Otherwise nimeteleza tu mpaka Dodoma
 
Wanakaaga na hapo ukimaliza kimara stand.. yani kama tunategena
Kuna siku washaniharibia safari,ile naanza wenge tu hawa hapa,nikajisemea hapa hapa dar naanza na mambo ya kuandikiwa vyeti,kufika misugusugu pambavu wengine tena wanakuonyeshea na picha kabisa ya speed yako waliotumiwa na mshashi anaepiga tochi,nikaona isiwe tabu ikabidi niwe mdogo tu safari yote,maana wanaweza kukufilisi wale jamaa
 
Back
Top Bottom