Wakuu nimesafiri salama kabisa. Nimefika Tanga Mida ya saa kumi na moja hivi. Kuanzia moro kwenda chalinze nilikuta msafara wa makamu wa rais, basi askari wakaturuhusu wenye magari madogo tutangulie. Magari makubwa yote yakazuiliwa na magari yote kutoka DSM kuelekea Morogoro yakazuiliwa. Basi tukajikuta barabarani tupo wenyewe tu na uelekeo ni mmoja na askari wanaelekeza kuwa tukimbie. Aisee nimekimbiza gari balaa, nimejikuta naenda hadi 170kph. Kuna mwamba ana Toyota crown athlete ametupita kama vile tumesimama. Na kuna jamaa ana raum nyekundu, aisee ameikomesha ile gari, alikuwa kama anapaa na vile tochi zote ziliondolewa