Kuna siku nilikua natoka dar kwenda bara. Nikapita mbezi kulikua na watu wengi saaana na gari ndogo nyingi Mida ya saa Saba mchanna.
Nika park wakanikimbilai vijana wanasema wana abiria wa Moro nikawambia nahitaji wa moja Kwa moja mpaka dom waksema hakuna hapo hao abiria wote ni wa Moro wanangoja abood zitoke Moro zije ziwabebe.
Wakati natafakari akatokea mbaba mmoja kavaa nguo za kimasai akaniuliza naenda wapi nikamjibu Dom, akauliza nauli ya Dom ngapi nikamtaji. Akasema yeye analipa nauli ya Dom lakini atashuka Moro na yupo na mwanae. Nikasema hamna shida.
Tuka Anza safari Yule Mzee WA kimasai alikaa seat ya mbele na mwanae nyuma. Nilianza kuona kero baada ya Mzee kuingiza mkono wake kwenye shuka lake na kukuna P***bu Kama vile yupo peke Ake chooni hivi ili bidi nizime AC tule upepo maana Hali ilibadilika. Mpaka tuna fika Moro Ile pesa yake ikabidi ninunue manukato.