Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Amen
Asante sana.

Wakati najinasua humo kwa mbali nikasikia sauti za wasamalia wema wakisema "njooni tutoe maiti humu hatotoka mtu" so ni muumba Tu alitenda miujiza yake. SIKUUMIA KOKOTE japo alie sababisha alikimbia
Pole sana mkuu.
Mungu ni mwaminifu,hutufanyia njia pasipo na njia.


Umenikumbukusha ajali yangu niliyowahi kupata,,watu walidhani nishapasuka fuvu..ila Mungu ni mwaminifu.


Mungu aendelee kukulinda mkuu,
Ajali isiwe sehemu yako tena🙏
 
Tumeuanza mwaka Ila kuna mtu sioni ski comment siku hizi. Bwana Extrovert kimya mno. Ingekua ni bwana RRONDO angesha tafutwa Kwa udi na uvumbe na hizi pic Kali.

Mm nilipata mzinga mwaka Jana nikapotea muda mrefuuu hakuna ATA alie ulizia hehe. Tumshukuru mungu tuko hai. Binafsi nimeuona uwepo wa mungu. Tukumbukane thou hatufahamiani.View attachment 2076423
Maisha hayako fair mkuu, kuna watu wazito humu [emoji1787][emoji1787]

Pole sana kwa mzinga mkuu, la muhimu uhai
 
Pole mkuu.

Mzinga kama huu sio wa kitoto.

Ila mara nyingi wale wanaouliziwa utakuta wanafahamiana na wadau wengine nje ya jukwaa.

Sasa ukikaa kijeshi kama mimi, siku ukipotea ni ngumu kuuliziwa.
🤣🤣🤣🤣
Mimi huwa nakuulizia mkuu.

Kabla sijakuona huu uzi,kuna uzi fulani tulionana nikakuchangamsha na wewe ukanichangamsha kwelikweli.
 
Back
Top Bottom