Nilikua natoka Dom - Arusha.
Kufika makuyumi huwa Kuna kizuizi usiku kwajili ya magari makubwa kukaguliwa, gari ndogo zina pita.
Baada ya kizuizi kuna mizani hivyo magari makubwa yakitoka kukaguliwa huingia mizani alafu yanaendelea mbele uelekeo wa Arusha.
Kumbe kuna gari kubwa moja walipita pale kwenye kizuizi kimagumashi Kwa kutoa ela ya kiwi kwasababu gari Lao bovu sanaa.
Ghafla nikalikuta halina taa hata moja, halina reflector na linatoa Moshi mwingi Sana wakati huo chombo imesha kubali gear na upande wapili kuna chombo ingine iko mafuta Sana.
Option niliyo Kua Nazo za haraka ni kuigonga Kwa nyuma Ile gari mbovu, kuigonga Uso Kwa uso Ile gari ilyo Kua inatoka Arusha au kulimwaga porini.
Mind you hapo barabara iko juu porini ni chini na kuna wanyama.
Basi nikalitupa huko porini likapinduka mara mbili lakini kabla nilisha hangaika na brakes gari ikawa ina sota Tu it was too late.
Alipo kuja mkuu wa kituo pale makuyumi aliwasema Sana wale police kwanini alishindwa kuifwata Ile gari kubwa kumbe washa Kula Chao.
Msaada mkubwa ulitoka Kwa maderava wa magari makubwa. Hawa WA gari ndo walikua wanapita shwaaaa shwaaaaaaa shwaaaaa
Ilikua hivyo.
Ni nadra sana kupata msaada ukiwa highway kutoka kwa madereva wa magari madogo , Hawa jamaa wa magari makubwa(malori) huwa na msaada sana aisee....big up kwao.Pole sana, hii ndio sababu sipendi kuendesha usiku. Kingine mtu akiwa anaendesha na mbele kuna lori au gari lolote anachochea tu ili alipite bila kujua kuwa unapoikaribia ile gari na mwendo wako mkubwa mbele inaweza kutokea gari ingine ushindwe kupita utaingia nyuma ya lori au porini.
Ni kweli kabisa watu wa malori ni watu wanajitoa sana kwenye majanga. Sisi wa magari madogo tunajiona tuna haraka zetu bila kujua kilomita chache mbele unaweza kuwa wewe unaehitaji msaada.