Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mara zote huwa wana maneno mazuri sana ila lete hio gari na ushahidi wako watakwambia sio sahihi na kukupa assessment Yao.
Kuna shida mahala, ila acha tupambane tu. Hata ushuru wa baadhi ya gari sio sahihi.. bora tungekuwa na kiwanda ndani ingekuwa sawa, kufanya ushuru juu.. ili kutubana tununue ya ndani
 
Kuna jamaa yangu kaisha anza nunu vitu, engine ilikufa sasa ameagiza engine ingine.. alichukua gari kutoka singapore
Singapore wanatabia kama za Kinondoni,Sinza na Magomeni hata ukinunua Toyota unakuwa mashakani, Kuna mtu alichukua Toyota Hiace Quantum yenye injini ya 1KD, injini ikaanza na tatizo la cylinder head.
 
Nafikiri huwa wanatoa vitu vizima wana weka vibovu, maana unakuta chuma imesimama kishenzi kumbe washachomoa engine na gear box.. wanakuwekea vya mtego mtego. Ila watu nao washtuke.. wanaonywa sana kuhusu Singapore
 
Ndiyo nilikuwa nimetoka zangu kumaliza driving school kujifunza manual then kesho yake nikachukua automatic nikaingia barabarani. Nikaenda na akili zangu za kimanual manual kwenye automatic nikajikuta nishaiva.

Sema wakati wa kuenda nilienda vizuri tu ila wakati wa kurudi sasa ndiyo nikatoa boko. Ilikuwa ni mitaa ya home tu nikiwa narudi ndiyo nataka nitoke kwenye lami nikunje kona niingie kushoto kwenye barabara ya vumbi inayoenda home.

Tulikokuwa tunaishi baadhi ya sehemu kuna ng'ombe na punda wengi wenyeji wanawatumiaga kubeba mizigo yao. Na huwa wanawachunga na kutembea nao barabarani hovyo tu hivyo kupishana nao kila siku ni jambo la kawaida.

Sasa wakati narudi ili nikaingie kwenye ile kona nilikuwa spidi nikajisahau kupunguza hivyo badala ya kukunja kona nikaenda nikagonga kile kizingiti cha kwenye kona. Vile ambavyo vinawekwaga kwenye kona pande zote mbili.

Vile vinajengwaga kwa zege na nondo halafu kwa chini kulikuwa na kamtaro kanapita. Kwahiyo nikagonga kile kikapinda kikawa kama kinataka kuingia kwenye mtaro then tairi ya upande wangu ikaingia kidogo kwenye mtaro.

Sasa pale kwenye kona karibu kabisa na ule mtaro palikuwa na ng'ombe anakula vimajani pale na mtu anayemchunga alikuwa pembeni yake. Yule mtu alipoona nimepoteza uelekeo akaruka akamuacha ng'ombe wake pale.

Sasa alipokuwa amesimama yule ng'ombe ndipo gari ilipoenda kugota kwahiyo ikampush yule ng'ombe akaanguka then number plate ikamkata kidogo kwenye mkuu. Sikuumia na gari ilitoka nzima ila tu bumper la mbele liliachia kidogo.
Ajali ni kitu cha ajabu..[emoji38][emoji38][emoji38]...tukio la ajali huwa halidumu zaidi ya sekunde mbili, tatu at most..[emoji38][emoji38][emoji38]
Ila ukiamua kuelezea vizuri ilivyokuwa unaweza ukaandika kakitabu..[emoji119][emoji119]
 
Hahaaa wengi niliowasimulia walikuwa wanacheka. Wengine baada ya siku kadhaa wakawa wananiuliza kiutani eti vipi ng'ombe wetu anaendeleaje.

Ninachoshukuru mtu aliyekuwa amemshikilia yule ng'ombe alipoona nimepoteza muelekeo akaruka pembeni akamuacha ng'ombe wake. Vinginevyo yangekuwa mengine.

Hapo ndo nimetoka zangu driving school kujifunza Manual kama leo then kesho yake nikachukua Automatic nikaingia barabarani. Nikajikuta Michael Schumacher huyu hapa hihiiiii.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila mommah bhana, aaaaah
 
Ndiyo nilikuwa nimetoka zangu kumaliza driving school kujifunza manual then kesho yake nikachukua automatic nikaingia barabarani. Nikaenda na akili zangu za kimanual manual kwenye automatic nikajikuta nishaiva.

Sema wakati wa kuenda nilienda vizuri tu ila wakati wa kurudi sasa ndiyo nikatoa boko. Ilikuwa ni mitaa ya home tu nikiwa narudi ndiyo nataka nitoke kwenye lami nikunje kona niingie kushoto kwenye barabara ya vumbi inayoenda home.

Tulikokuwa tunaishi baadhi ya sehemu kuna ng'ombe na punda wengi wenyeji wanawatumiaga kubeba mizigo yao. Na huwa wanawachunga na kutembea nao barabarani hovyo tu hivyo kupishana nao kila siku ni jambo la kawaida.

Sasa wakati narudi ili nikaingie kwenye ile kona nilikuwa spidi nikajisahau kupunguza hivyo badala ya kukunja kona nikaenda nikagonga kile kizingiti cha kwenye kona. Vile ambavyo vinawekwaga kwenye kona pande zote mbili.

Vile vinajengwaga kwa zege na nondo halafu kwa chini kulikuwa na kamtaro kanapita. Kwahiyo nikagonga kile kikapinda kikawa kama kinataka kuingia kwenye mtaro then tairi ya upande wangu ikaingia kidogo kwenye mtaro.

Sasa pale kwenye kona karibu kabisa na ule mtaro palikuwa na ng'ombe anakula vimajani pale na mtu anayemchunga alikuwa pembeni yake. Yule mtu alipoona nimepoteza uelekeo akaruka akamuacha ng'ombe wake pale.

Sasa alipokuwa amesimama yule ng'ombe ndipo gari ilipoenda kugota kwahiyo ikampush yule ng'ombe akaanguka then number plate ikamkata kidogo kwenye mkuu. Sikuumia na gari ilitoka nzima ila tu bumper la mbele liliachia kidogo.
Poleeeeh sana mommah [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukinipiga full, nami nakupiga full.
JamiiForums1911020241.jpg
 
Mashamba ya chai barabara ya Njombe -Ludewa, kuelekea ziwa Nyasa.

Kuna mlima mmoja wameweka barabara ya zege wachina sasahivi, yani uko kama test tracks. Kona za kutosha kupima stability na straights za kutosha kupima msuli. Plus adrenaline junkies unawafaa maana kona zake japo ni pana ila kuna points nyingi tu ambazo ukikosea unaporomoka.

Naifananisha kwa utamu na ile ya Dodoma Babati, hasa mle mlimani ila hii pana zaidi na ina kona kali mithili ya Nyangoro.

Hii nchi tamu sana, pigeni trip wakuu

20220122_130330.jpg
 
Back
Top Bottom