Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kupata average 110kph kuna sehemu inabidi ufanye hivi....
View attachment 2135131
Bila shaka. Na watu walikuwa wanapiga stori kwenye gari na kuongea na simu as if niko 100 kumbe niko 180.

Abiria mmoja alikuwa anatapika njia nzima. Next time nikipakia abiria nawauliza kwanza kama wako stable maana ilikuwa patashika.
 
Sasa unaingia mkoa wa Mara!!
Hahaha umenikumbusha hii
Ila wabongo dah
Eti be strong
JamiiForums1690879257.jpg
 
Bila shaka. Na watu walikuwa wanapiga stori kwenye gari na kuongea na simu as if niko 100 kumbe niko 180.

Abiria mmoja alikuwa anatapika njia nzima. Next time nikipakia abiria nawauliza kwanza kama wako stable maana ilikuwa patashika.
Hio siwezi kushikilia. Huwa nagusa nikitaka kumpita mtu mbishi, matairi yenyewe ya kichina!
 
Mimi nikishaifikia nalegeza mguu kidogo rpm ishuke mpaka 4000 ambayo ndio ina maintain 180kmph kwenye flat road.

Hilo la matairi, ndio maana nasemaga bora kuna limiter tu, 180 inatosha kibongo bongo kwa matairi tunayouziwa nchini.

Nimetumia tairi one year, imeshaisha. Natakiwa ninunue viatu vipya nikirudi hii trip.
 
Kurudi muda mwingi nimetembea 120-130kph very relaxing speed.
 
Heri ningemalizia hizi km200 jana nikafika Musoma. Kiherehere changu kusafiri asubuhi nimeliwa fine mbili back to back zimepishana nusu saa.

Shikamooni wakurya, mmenikaribisha vilivyo kanda maalum

View attachment 2135114
Nilijua

Hutoboi bila cheti[emoji1787]

Pale mkula kuna down kuelekea lamadi

Wana kiherehere sana wale jamaa wa za ku brush viatu

Pale manyamanyama

Na unapoingia makutano[emoji1787]
 
Kurudi muda mwingi nimetembea 120-130kph very relaxing speed.
Na consumption nzuri. Kutoka Moro mpaka Musoma nimeenda 9.5 kmpl, nilikuwa naishi kwenye 130 na 140, mara moja moja akitaka mtu kuleta dharau ndo nilikuwa namaliza kisahani.

Kuna GRS200 iliniletea dharau jioni Karibu na Singida, akaomba ligi. Kuna jambo kajifunza.
 
Nilijua

Hutoboi bila cheti[emoji1787]

Pale mkula kuna down kuelekea lamadi

Wana kiherehere sana wale jamaa wa za ku brush viatu

Pale manyamanyama

Na unapoingia makutano[emoji1787]
Nimeliwa somewhere vijiji kama vitano baada ya Old Maswa, jamaa hakuwa na karatasi akaniambia nitalipa mbele. Nilikuwa nachill na 65 sema ndio hivyo.

Huku nikiendelea kutafakari na kusali labda mashine imemgomea, pale Serengeti one stop kwa mbele ni Eneo la Mbuga aisee. Jamaa akanivuta akanitaarufu nimevuka spidi yao ya mbugani. Nikamuambia nimetoka kuandikiwa sahizi niangalizie. Kaniprintia ya mwenzie afu kaongezea na yake hapo, kanipa na pole [emoji1787][emoji1787]
 
Jana kuna Jamaa wa lori kaniokoa kula cheti. Maeneo ya Mwanga kuna ka lami kapya Jana kuna sehemu walitega. Bila jamaa wa Lori kunishtua wangenipa cheti maana nilinogewa.
 
Lembeni pale

Ukishaanza kupanda kuna 50kph

Wanaoteaga hapo

Ama pale njiapanda ya nyumba ya mungu

Halafu wanajiona( ga) majeshi majeshi sana

Wanakera
 
Nimeliwa somewhere vijiji kama vitano baada ya Old Maswa, jamaa hakuwa na karatasi akaniambia nitalipa mbele. Nilikuwa nachill na 65 sema ndio hivyo.

Huku nikiendelea kutafakari na kusali labda mashine imemgomea, pale Serengeti one stop kwa mbele ni Eneo la Mbuga aisee. Jamaa akanivuta akanitaarufu nimevuka spidi yao ya mbugani. Nikamuambia nimetoka kuandikiwa sahizi niangalizie. Kaniprintia ya mwenzie afu kaongezea na yake hapo, kanipa na pole [emoji1787][emoji1787]
Kutoka old maswa..

Nyakabindi

Igaganulwa (dutwa)

Mkula halafu Lamadi

Cheti

Ulipigiwa mkula simiyu

Ulivyovuka rubana bridge tayari

Pale mizani ulishaianza kanda maalum

Kwenye lango la kuingia serengeti
 
Back
Top Bottom