Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Labda utoke D uje D2 Kwa muda then ujimalize na L na hand brake Kwa mbaaaaaali
Kuna Toyota Noah, nimewahi ikuta Mkamba, njia ya Kilombero Ifakara. Dereva analalamikiwa kasimama mbele kushusha raia, akawa anajitetea gari breki hazikamati na ni Auto.

Tuliongozana nae mida ya jioni, speed aliyokuwa anatembea sio mchezo na abiria kajaza mpaka kwenye buti. Kona za Mangula,mitaa ya Kiberege anavyotembea ni hatari
 
Moja ya maeneo napenda sana kupiga picha...

Mara ya kwanza kupita hii mahali ni enzi hizo za kina Kwacha, Kiswele na hadi sasa mandhari yake haijawahi badilika...

Hili ndio eneo linalotenganisha nyanda za juu kusini na uwanda wa chini wa pwani, eneo linalotenganisha baridi ya kusini na joto la pwani...

Kitonga moja

View attachment 2442005

Msalimie Msafiri 😊.

Mwambie asiniache safari hii kwenye Nissan Safari yake....☺.
 
Kasinde mpenzi umekuwa adimu sana...huko Butiama kuingia jeiefu inahitaji visa eenh 😁?

Salamu zimemfikia naye kauliza kama nilivyouliza hapo juu...

Aahahahahaaahahaaa waaalaaah, VISA ya humu sina mipaka nayo, sema tuu nikisahau nilipoweka miwani yangu ndo basi tena humu siwezi kuinhia na kusoma au kuandika...😅😅😅

You are missed than the way I miss goody goody toffy....😋😋😋😋

Sugar sugaring thing.....

Before new year twende mahala penye tutafanya cheers ya fruti fruti......

Yaani tule matunda weeeh hadi nami nikuwe sukari kama wewe...😅😅

Niko sirias....
 
Unaendesha gari kubwa au ndogo. Kama upo Dar nenda jengo la Maktaba Square Posta uliza ofisi za In Transit Drivers Association (ITDA) upeleke maombi yako saizi wamekula shavu la kutoa gari bandarini na kupeleka bandari kavu (ICD).

Kama ni maroli piga namba hii kisha jielezee wanataka madereva 0677469840
Asante Kaka nitafanya hivyo
 
umeandika jambo zuri sana ila sidhani kama wahusika wataliingiza kwenye vipaombele vyao.

mimi nalia na mamlaka zenye dhamana na masuala ya utalii. ekolojia ya maeneo yenye miiniko kama mlima kitonga ni very potential kwa utalii. huu mlima ukiachia ile sifa yake mbaya ya ajari za gari, ni kivutio kizuri sana.

ilitakiwa pawepo na hotel nzuri ya kitalii eneo lile la mlima. ingevutia sana wageni wanaopenda kufanya camping, hiking/trekking, adventure, nature photography nk.

sijui kwanini nchi yetu inasuasa kugeuza maeneo kama haya kuwa vivutio vya utalii.
Kwa huu utamaduni mpya wa nyumbani kwanza ni vigumu kupewa kipaumbele sehemu ambayo kiongozi hatoki huko,ni mchezo hatari sana kwa usalama wa nchi.
 
Tatizo la nchi yetu kila kitu kinahitaji political will na sio wataalamu waje na plans na ziwe implemented, kuna mzawa alijaribu pale Comforts Hotel ,pass inapoanzia ukitokea Ruaha, hoteli ikavuma na ikaja pasuka,ule mlima kuna potential nyingi mno za kiuchumi including kutoa ajira hasa kwenye hiyo sector ya utalii, kuanzia hiking, jumping, kayaking [emoji1629], tourist camps, wenzetu Zambia wanazo hizi camps nyingi tu,T1 nzima naona tuna hii camp moja tu,pale iyovi inapoanzia ukitokea mikumi, ni shame hasa nchi yetu hii
Ukipita kipindi cha masika ile greenish inavutia sana!
 
moja kati ya back to back roadtrip nilizowahi kufanya ni ya dar-bukoba.

hii ilikuwa ni june 2020. video nilitengeneza kwa msaada wa application mbili ambazo ni google map na google earth.

nilichofanya, wakati tumebakiza kilomita chache kuingia bukoba, nilichukua simu yangu, nikawasha gps, nikaingia google map, nikaset direction. baada ya hapo nikafanya screen-recording kwenye simu yangu.......the end result is amazing.

NB: ktk teknolojia ambayo ninai-utilize at 100% when i'm on a roadtrip, is goople map and google earth. waliovumbua hizi application mbili Mungu awashushie baraka maradufu.

tazama video.
 
Mwezi wa 12 Tar 17 mwaka jana niliweka Hydrolic oil (gearbox) na nikatoka Dar kwenda Mwanza..Km 1000+
Baada ya hapo Gari imeenda karibu Km 1500 zingine,

December Hyo nilimwaga Engine oil pia na Nikaja tena Kumwaga mwezi wa 9 Mwaka huu..hapo chini ndo aina ya Oil nazotumia...gari Ni Premio X..

Nna safari ya Arusha hivi karibuni, Je natakiwa kubadili hizi oil tena?
IMG-20211213-WA0022.jpg
20221212_161857.jpg
 
Kwa manual kuendesha bila brake unakuwa comfortable maana engine braking inatosha. Ila kuna miamba wanaendesha automatic car yenye breki mzozo au bila breki
Automatic bila brake hapana kwa kweli sitaki hata kusikia. Nakumbuka kuna mzee mmoja hivi alikuwa na Landrover 109, ile gari aliitoa brake & clutch pedal.
 
Back
Top Bottom