Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Screenshot_20230105-224301_1673024179494.jpg
 
Baada ya mwaka inarudi jikoni inapigwa body service na rangi mkono mmoja..anapewa dalali anampata mtu anaehisi amebahatisha probox kwa 5m.

Anakuja kujitamba humu JF na ndo gari yake ya kwanza..
Week ya kwanza gari innanza kusumbua anarudi tena humu kuomba msaada wa fundi mzuri[emoji23]

Mara gari haiwaki mara inazima ghafla anaamua kupaki na kuyachukia magari moja kwa moja[emoji119]

Nasisitiza kuwa makini na gari za mkononi.!
 
Clever
 
Nilimfanyia mtu roho mbaya juzi hapa. Crown nyeupe DYA barabara ya Babati - Dom. Kanikuta naovertake lori kanikalia kooni nimpishe nikasogea mdogo mdogo akasepa kwa jeuri.
Wakati huo nimejisahau kujaza mafuta Babati na sikuwa na uhakika sheli itapatikana wapi, so mdogo mdogo ndo mwendo maana ligi bila wese ni maumivu.

Nimefika Kondoa nikajaza mafuta, jamaa alikuwa amekaa round about kushoto kapaki. Alivyoniona nimepita akaingia kwa nguvu barabarani anifukuzie, mimi nilimkumbuka nikammonitor kwenye side mirror. Barabara yenyewe haina magari huwezi kumsahau mtu.

Kanifikia mpaka kwenye bumper kaanza kuniwashia mataa, ikabidi nimpe anachokihitaji.

Mlima wa kwanza wa pili, mtu hayupo kwenye side mirror. Kitendo cha dakika kama mbili maximum. Milima ile niliigeuza tambarare napanda na 180 ni limiter tu mshale haushuki chini.

Baada ya kuhakikisha haonekani kabisa, nikarudi mwendo wangu wa 100 - 120, aliponifikia nikamwacha maana alikuwa hapoi, ila nilihakikisha ujumbe ameupata. Hata kama nina budget mafuta usinifanyie dharau.

Itakua alitamani kujipima ubavu na gari yako.
 
Back
Top Bottom