Ohoo pole sana kaka, lakini pia uwapo barabarani jitahidi kutumia na lugha za ishara kidogo...
Mfano kabla ya kuli overtake lorry, unaweza kumshitua kwa kumpigia horn ya kuibia kidogo, hii itamfanya dereva lorry akuzingatie na akupe nafasi ya ku overtake kwa wakati (angalizo, usije ikampigia horn ya fujo kama ile ' Piiiiiiiiiiiiiii... Piiiiiiiiiiiiii... Piiiiiiiiiii... hapana, ni Pipip.. Pipip...)
Alafu unaongeza na kumuwashia taa na kuzima, bila kusahau kuwasha indicator. Hiyo ya taa itampa ujumbe hadi Hiace kwamba nawewe una overtake kidogo, kwahivyo alegeze goti kidogo kukupa nafasi.
Mwisho kabisa jitahidi sana sana sana kuwa na nidhamu barabarani, overtake nzuri inahitaji nodhamu kubwa sana, hakikisha unaona mbele vizuri na hakuna chombo kilicho karibu.
Pia zingatia kukijua chombo chako na uwezo wake, unaweza kuona lorry limebeba container ya 40ft kumbe ni empty container na lorry ikawa nyepesi kuchanganya kuliko uwezo wa chombo chako.
Hakikisha unatengeneza timing nzuri ya kufanikisha overtaking ndani ya muda, usibweteke kwa kuona 40ft container kuidharau lorry [emoji597], itakuja kukushangaza siku moja.
Pole sana ndugu na nikutakie kheri zaidi uwapo barabarani.
Mwisho kabisa nawakumbusha madereva wenzangu kuongeza umakini na kujenga nidhamu barabarani.
Sent using
Jamii Forums mobile app