Uuweeeh....!!! Mi licha ya umri kusonga namuiga Baba Bataringaya 🙌.
Nimestaafu mambo ya kiza kinene, nyie endeleeni kutuwakilisha.
Wee lile giza la kwenye yale madaraja ya kati ya Bagamoyo na Msata unalionaga.....
Halafu ile siku napita sikupishana na gari yeyote toka Msata hadi nafika kituo cha mafuta BP, weeeh.... sina hamu.
Wakati najaza mafuta tena ile usiku mnene pale BP nilikuta Nissan Patrol zile tinted (za kazi maalum za kiserikali) niliitambua haraka japo ina plate namba za kawaida.
Dereva alikuwa ananitolea macho yenye maswali ila hana namna ya kuniuliza....
He was like, wewe mwanamke, usiku wote huu unatoka wapi, halafu nilivokuwa nimevaa sasa.... kilemba gauni kama dera ila linaishia magotini, viatu chachacha za ngozi soli ya mpira ile inakunjika kama silicon....🤪🤪🤪
Nikawa najinyoosha maana ndo sehemu niliona salama kushuka tangu kuanza safari Tanga, kisha huyooo nikamalizia safari hadi kitongojini nikapumzisha Bange za Kasinde.