and 100 others
JF-Expert Member
- Feb 3, 2023
- 3,707
- 12,367
Miaka ya nyuma sana, ndani nilikuta kitabu , kile kitabu kiliandikwa kama mashairi flani na wazee wa kiislamu wakiomba Sadam Hussein aliyekuwa rais wa Iraq anyongwe.Ndio maana ikaitwa ni shirki.
Kwasababu kuna kitu nje ya dini unakifanya japo unatumia maandiko yake.
Ilikua kabla hata ya US kuivamia Iraq, ni kijitabu kidogo nilikisoma juu juu nikakiacha.
Baada ya Saddam kukamatwa na US akanyongwa kweli.
Hapo niliamini ..maombi yapo.
Nilikitafuta kile kitabu sikupata kukiona tena, nahisi kilikua cha mzee wangu.
Kitabu kizima kilikua ni maombi ya Saddam Hussein anyongwe.