Wazee wa UCHAGANI, mkumbusheni Rais Samia mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji

Moshi wa kuifananisha na tanga nenda huko
 
hata mimi hapa nilikuwa najiuliza sana ujue" huyu jamaa amepata wapi ujasiri wa kuifananisha Mbeya na Moshi? Moshi itasubiri sana kwa jiji la kijani (Green City)
Si ndo hapo ndugu yangu!!,Kweli mtu akutukanae hakuchagulii tusi.
 
Uchagani huyu ndiye rais wa mioyo yetu,hatusikii hatuambiwi,Acha kabisa lekha kabisa meku,Yaani huyu #samia ndiyo rais mpaka #2040 bhaba yangu,hata ufanyeje,na tumeanza kuipenda CCM ile mbaya,nadhani labda umeisemea #babati na chuki zao.
Hakuna mchaga mjinga kama wewe
 
Aridhi si ya serikali ikiamua kuichukua kwaajir ya maendeleo ya jamii utachukua na kuwalipa fidia
 
Kwaiyo hakuna maduka makubwa na showroom?
 
Huku uchagani hatutaki hata kumuona huyu bibi
😂😂😂😂

Weee mmang'ati muiraqwi mtumwa wa mbowe, sasa umeanza kutamani kuwa mchagga😂😂😂😂

Mmerogewa nini aisee jamaa
 
Uchifu uendelee hayo ni maoni yake. Huyu ni Mtanzania mhindi?
 

Mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji au Mji wa Moshi unapaswa kuwa jiji?
Fafanua kwanza kisha tuchangie
 
Wachaga wajanja sana. Yaani kazi yao ni kwenda mikoa mingine kujazana tu huko na kununua Ardhi lakini kwao hawataki kuuza Ardhi. HII NI AKILI KUBWA KAMA WAYAHUDI. Nadhani vizazi vijavyo huko mbeleni ndio wataelewa na kuwapongeza babu zao
Hakuna kitu kama hicho. Dunia inaenda kuwa kijiji, kadri tunavyoenda mbele teknolojia inakua na mambo ya kijima yanapotea.

Hakuna siku itafika kwamba wachaga wote watarudi nyumbani kugawana ardhi wabaki hapo wapambane kufanya maendeleo.😂😂.

Msiposhirikiana na Watanzania wengine kuleta maendeleo kama wao walivyowaruhusu mpeleke maendeleo kwao uchagani kutaendelea hivyo hivyo mwishowe ardhi ya uchagani itabaki kuwa sehemu ya kuzikana na kutembelea mwezi wa 12.
 
ukiondoa usafi hakuna kitu kingine moshi ilichoipita moro kuhusu majengo marefu moro ni babalao
 
Wakati mwingine uwe unasafiri uone nchi ujue miji ilivyo....
Jina la akaunti yako hapa jf linasadifu ulivyo shallow minded. Unajuaje kwamba sijasafiri hii Tanganyika au wewe ni mpiga lamri? Ili Manispaa ipewe hadhi ya jiji huwa kuna vigezo vingi tu vya msingi vilivyoainishwa kisheria. Sasa badala ya kutu-convince kwa kutuonyesha jinsi manispaa ya Moshi ilivyokidhi vigezo vyote/vingi vinavyotakiwa lakini inabaniwa na serikali kuwa jiji wewe una leta maneno matupu tena mbofumbofu. Kama ingekuwa ni rahisi hivyo basi Morogoro na Iringa zingekuwa zilisha kuwa majiji muda mrefu.
 
Hakuna cha vigezo wala nini, Dodoma ilitangazwa na Jiwe kuwa jiji bila kutimiza vigezo. Njia iliyotumika kwa Dodoma kwa nini isitumike kwa Moshi?
Kama tukijenga utamaduni wa namna hiyo wa Rais aliyeko madarkani kuacha kuzingatia vigezo na kufanya kwa mapenzi yake basi Manispaa zote zitakuwa majiji sasa. Nadhani kwa Dodoma japo kuna baadhi ya vigezo yawezekana vilikiukwa lakini yale maamuzi yaliendana na kuendeleza Dodoma kama makao mkauu ya nchi na ndiyo kazi inayofanywa sasa hivi ya kuijenga Dodoma. Hata Hivyo sikubaliani na kukiuka vgezo vya kisheria vya kifanya manispaa kuwa jiji. Dodoma ilitakiwa kuendelezwa kwanza ndiyo ipandishwe hadhi ya kuwa jiji.
 
Ikiwa Katiba yenyewe haifuatwi ndiyo itakuwa hivyo vigezo. Ule mkoa mpya unaopigiwa jaramba uanzishwe kule katikati ya Kitovu cha utalii una vigezo kushinda Tabora na Morogoro??
Hukumsikia Hangaaya akisema kwamba kama vigezo vikitimia ndio utafanywa kuwa mkoa? Hata huo aliyekuwa anataka kulazimisha kuufanya kuwa mkoa asingeweza kufanya hivyo bila vigezo kuwepo ndio maana alikuwa analazimisha baddi ya mambo kama airport, hospitali kubwa, taasisi za serikali kama vyuo n.k. Yote haya alikuwa anayafanya ili kutafuta vigezo vitimie.
 
suala la vigezo moshi ilishakuwa navyo kitambo. Kamuulize Jafo atakwambia hata yeye alishangaa kwa nini magufuli hakuipaisha moshi kuwa manispaa kwa sababu ya chuki zake za kisiasa akaipaisha dodoma ambayo mpaka sasa japo wamehamia huko bado haija kidhi. na wakati huo moshi ilishapeleka maombi lakini dodoma haikuwa imepeleka maombi iwe jiji.....it seems wewe ndiye uko shallow minded and less informed.

kwani morogoro na iringa zikipewa hadhi ya jiji kuna shida gani? Moshi, morogoro, Iringa au Tabora zimepungukiwa nini dhidi ya Tanga au Dodoma zilizopewa hadhi ya jiji?

you still need to learn a lot. nchi hii huijui wewe
 
Kwa hiyo serikali haitaki kwa makusudi kuifanya manispaa ya Moshi kuwa jiji? Weka hapa vigezo wacha mineno mingi! Otherwise just continue to live in your fantasies!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…