Wazee wa UCHAGANI, mkumbusheni Rais Samia mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji

Wazee wa UCHAGANI, mkumbusheni Rais Samia mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji

Wewe kila kona unatukana watu! Hivi hiyo moshi ina nini cha maana haina mzunguko wa fedha,haina maendeleo imedumaa miaka nenda rudi pia imejaa ukabila!
Mkuu, ni vyema uandike unachojua au kukifahamu, Moshi ya 2000 sio Moshi ya 2020 tambua hilo.
Moshi ni kubwa na pana kuliko unavyofikiria, ukienda pembezoni vijijini unadhani uko 'vimji vidogo' kutokana na mpangilio na barabara kufika kwa kila kaya!
Moshi ni zaidi bro acha hizo.
 
Lete vigezo vinavyokufanya useme kwamba manispaa ya Moshi inatakuwa kuwa jiji. Bila kuleta vigezo vyako huu uzi utakuwa useless.
Ikiwa Katiba yenyewe haifuatwi ndiyo itakuwa hivyo vigezo. Ule mkoa mpya unaopigiwa jaramba uanzishwe kule katikati ya Kitovu cha utalii una vigezo kushinda Tabora na Morogoro??
 
Wazee wa UCHAGANI, mkumbusheni Rais Samia. Mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji.

Mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji ili kuweza kule maendeleo Kwa mkoa na Taifa Kwa ujumla

Hi dhana Kwamba wachaga watakuja kuitawala TZ , ni mawazo ya kijamaa ambayo ni ujinga mtupu.

Huu ujinga umesababisha mkoa wa Kilimanjaro kudumaa kiuchumi. Hebu fikirieni mkoa wa Kilimanjaro ungekuwepo Kenya. Ungekuwa hivi ulivyo hapa TZ

Serikali ina Sera mbaya Sana, mbovu za maendeleo, utasema nchi haina wasomi waliobobea kwenye uchumi.
mkoa wa Kilimanjaro au mji wa Moshi?
 
Na Professor Issa Shivji

Kwani uchifu ni utamaduni wetu? Makabila mengi hawakuwa na wachifu. Waliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao (km Wazanaki). Uchifu ulipigwa marufuku na sheria mnamo 1962. Machifu waliyokuwepo (km Adam Sapi, Fundikira, Kunambi nk) waliingizwa Serikalini katika nyadhifa mbalimbali.

Ufutaji wa uchifu ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa.Nchi zingine Za Afrika (kmNigeria, Ghana nk) wamepata shida kujenga umoja wa kitaifa. Sababu mojawapo ni machifu kulinda himaya zao kwa kukuuza ukabila badala ya utaifa. Tunachotakiwa kusisitiza ni utamaduni wa kitaifa.

View attachment 2091096
alipovikwa cheo cha Hangaya kule Sukumaland hamkukosoa!
 
morogoro napo utasema mjini? inawezekana hata kwenye top 10 ya miji bora tanzania wasiingie! moro mtasubir sana
Sasa moro utalinganisha na kijiji cha moshi kweli? Hujatembea moro wewe. Mimi coni ajabu mchagga kucfia na kusema moshi ni bora kuliko Dubai 😆but co wote
 
Huku uchagani hatutaki hata kumuona huyu bibi
Uchagani huyu ndiye rais wa mioyo yetu,hatusikii hatuambiwi,Acha kabisa lekha kabisa meku,Yaani huyu #samia ndiyo rais mpaka #2040 bhaba yangu,hata ufanyeje,na tumeanza kuipenda CCM ile mbaya,nadhani labda umeisemea #babati na chuki zao.
 
Suala la kuwa Jiji litafanikiwa tu japo kuna vigezo lazima vizingatiwe, kwani hata Rais aliyepita mwaka 2020 aliwahi kuzungumzia hilo, mojawapo ni eneo la manispaa kuwa dogo lakini wakimega kutoka kwenye wilaya jirani itawezekana.

NB: huyu mkulu wa sasa anataka nae aache legacy hivyo lazima tu atalifanya kuwa jiji ili apate cha kukumbukwa hahahah, hivyo komaeni nae , 2025 haifiki bila Moshi kuwa Jiji, Mark my words.
Bora ya Iringa kuliko Moshi
 
Hakuna cha vigezo wala nini, Dodoma ilitangazwa na Jiwe kuwa jiji bila kutimiza vigezo. Njia iliyotumika kwa Dodoma kwa nini isitumike kwa Moshi?
haiwezi kutumika kwa Moshi! Jiwe aliitangaza Dodoma kwasababu Dodoma ni mji wa kiserikali na ndio maana serikali ikaamua kuelekeza nguvu pala na mpaka hivi sasa kama utakuwa umetembelea siku za hivi karibuni utaona jinsi ilivyobadilika na sasa ni jiji la 4 kwa hapa bongo
 
Sasa moro utalinganisha na kijiji cha moshi kweli? Hujatembea moro wewe. Mimi coni ajabu mchagga kucfia na kusema moshi ni bora kuliko Dubai [emoji38]but co wote
mi sio mchaga .....na moro naijua vizuri sana sababu ndio my current city, ila ukweli lazima niongee " Moro bado sana sababu naijua vizur sana huenda ikawa tofauti na unavyoijua wewe
 
Uchagani huyu ndiye rais wa mioyo yetu,hatusikii hatuambiwi,Acha kabisa lekha kabisa meku,Yaani huyu #samia ndiyo rais mpaka #2040 bhaba yangu,hata ufanyeje,na tumeanza kuipenda CCM ile mbaya,nadhani labda umeisemea #babati na chuki zao.

[emoji3][emoji3][emoji3]
Nimecheka sana, inaonekana hapo ulipo unaneemeka haki
 
mi sio mchaga .....na moro naijua vizuri sana sababu ndio my current city, ila ukweli lazima niongee " Moro bado sana sababu naijua vizur sana huenda ikawa tofauti na unavyoijua wewe

Washauri watoe viwanja kwa wageni/wazawa makabila tofauti waone kama hapatabadilika.
 
mi sio mchaga .....na moro naijua vizuri sana sababu ndio my current city, ila ukweli lazima niongee " Moro bado sana sababu naijua vizur sana huenda ikawa tofauti na unavyoijua wewe
Moshi iko vizuri sana sasa hivi. Barabara mjini nyingi kama siyo zote zina lami, majengo mengi ya ghorofa yamejengwa tofauti na zamani, kuna mpangilio mzuri wa barabara na majengo, na usafi wa hali ya juu. Morogoro ni kama imesimama hakuna maendeleo ya maana.
 
Tuma picha tuone
 
Mkoa mzima hauwezi kuwa Jiji.Jiji sio hadhi ya kiutawala,ni hadhi ya kimaendeleo ya eneo husika.Mwanza kama eneo ni jiji lkn sio Mkoa wote wa Mwanza ni jiji.Moshi inaweza kuwa jiji Ila Kilimanjaro haiwezi kuwa jiji yote.
 
Moshi iko vizuri sana sasa hivi. Barabara mjini nyingi kama siyo zote zina lami, majengo mengi ya ghorofa yamejengwa tofauti na zamani, kuna mpangilio mzuri wa barabara na majengo, na usafi wa hali ya juu. Morogoro ni kama imesimama hakuna maendeleo ya maana.
mkoa wa morogoro umelaaniwa ni vigumu sana kupiga hatua
 
Wazee wa UCHAGANI, mkumbusheni Rais Samia. Mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji.

Mkoa wa Kilimanjaro unapaswa kuwa jiji ili kuweza kule maendeleo Kwa mkoa na Taifa Kwa ujumla

Hi dhana Kwamba wachaga watakuja kuitawala TZ , ni mawazo ya kijamaa ambayo ni ujinga mtupu.

Huu ujinga umesababisha mkoa wa Kilimanjaro kudumaa kiuchumi. Hebu fikirieni mkoa wa Kilimanjaro ungekuwepo Kenya. Ungekuwa hivi ulivyo hapa TZ

Serikali ina Sera mbaya Sana, mbovu za maendeleo, utasema nchi haina wasomi waliobobea kwenye uchumi.
Una maana ya mji gani? Mkoa haiwezi kuwa jiji!!!
 
Back
Top Bottom