Iwapo mama samia au hata waziri wa michezo atatoa maamuzi juu ya kesi hiyo basi kitachotokea kitaitwa”SERIKALI KUINGILIA MPIRA WA MIGUU”
Kosa hilo likiwafikia wakuu wa soka FIFA,tff inakula ban kama ligi ya zimbabwe..
Coz ni marufuku serikali kuingilia maamuzi ya chama Au shirikisho la soka nchi yoyote ma adhabu yake huwa kubwa.
Ikumbukwe Wazee wa yanga walishawahi kutaka kuonana na mama samia ila nadhani hawakufanikiwa.
WAZEE WA YANGA MTAUPOZA MPIRA WA BONGO.
Hao Wazee hawajajikusanya Wenyewe bali ni Jeuri wanayopewa na Mstaafu wenu wa Mkoa wa Pwani ambaye ana Influence Kubwa ya Kiushawishi katika Awamu hii pamoja na Mama Karume kutoka Kwao Kisiwani Zanzibar.
Wanachokifanya hapa hawa Wazee ni Kumlazimisha Mama nae awapende na awapendelee Yanga SC ili iwe ni Kazi rahisi kwa Wanayanga walioko Serikalini akina Waziri Nchemba, Mzee Mkuchika, Manaibu Mavunde na Ridhiwani nao wasaidie katika Kumshawishi ili Rais wa TFF Karia atishwe na Kamati ya Maadili ya TFF itengue hiyo Adhabu.
Niliwahi kuonya huko nyuma kuwa Rais Samia akae mbali na kulazimishwa kuwa ( awe ) mwana Yanga SC kwani itakuwa na Athari Kubwa Kwake Kiutawala, Kiushawishi na hata Kiusalama vile vile kutokana na Nguvu Kubwa ya hivi Vilabu viwili ila sikueleweka na Wapumbavu wengi ila taratibu nilichokiona sasa kinakuja.
Anayeharibu Mpira wa Tanzania kwa sasa kwa kupitia Kampuni yake inayosimamiwa na GSM ni Mstaafu wenu wa Kikatiba kutoka Mkoani Pwani na asipoangalia au Watu wa TISS wasipoliingilia kati kwa kuacha Haki itendeke, Sheria zifuatwe na Mpira uchezwe kuna Machafuko makubwa na Hatari fulani GENTAMYCINE naiona.
Sisi wana Simba SC tunawasubiri tu wamalize Kuhangaika na huu Upumbavu Wao mkubwa ila Rais Samia akikubali tu kuingia katika huu Mtego anaotegwa na hawa wana Yanga basi ajue Safari yake ya kuwa Rais itakuwa na Misukosuko mingi, ataathirika mno Kisiasa na atakuwa ameshaleta Mpasuko mkubwa wa Kisiasa nchini kwani nasi wana Simba SC tutaamua kuwa kwakuwa Yeye anaipendelea Yanga SC kutokana na Rangi zake Kufanana na za Chama chake cha CCM basi nasi Simba SC tutakubaliana rasmi Wote tuwe wana CHADEMA ambao 85% ya Rangi yao ( zao ) inafanana na ya Klabu ya Simba.
Namalizia kwa Kukuuliza Swali ni kwanini Kipindi cha Hayati Rais Dkt. Magufuli Maamuzi kama haya dhidi ya Yanga SC yalipokuwa yakitokea ulikuwa ( hukuona ) hawa Wazee wa Yanga SC wakitishia kwenda Kuonana nae ( Hayati Rais Dkt. Magufuli ) pale ( hapo ) Ikulu?
Siasa ni Siasa na Soka ni Soka sawa?