Wazee wa Yanga wanaomba kukutana Rais Samia kulalamikia adhabu ya Manara..Wanajua madhara ya kitendo hicho?

Huyo Mama wa maridhiano si ajabu akakutana na hao wazee na akabatilisha adhabu.

Lakini hii hofu ya kufungiwa imekuwa ikitumiwa vibaya na viongozi wa mashirikisho ya mpira.
Siyo hofu bali ni fact Serikali ikiingilia maamuzi ya vyombo husika vya soka FIFA watatupiga tofali.
 
Tanzania Football Film.
Soka liingie rasmi kwenye siasa.
 
Haji hawezi kukwepa adhabu ya kufungiwa kwa sababu anarudirudia haya makosa anajua akipigwa faini yoyote ana uwezo wa kuilipa. Unakumbuka alivyokuwa Simba alipigwa faini ya milioni tano na uliona alivyokwenda kwa jeuri kuilipa tena akiongozana na msululu wa waandishi wa habari.

Nia ya adhabu ni mhusika ajutie kosa lake na ajirekebishe na si kumkomoa. Sasa akipewa faini hata ya milioni 90 kuna watu watamlipia unafikiri anaweza kujutia kosa lake na kujirekebisha. Adhabu ya kifungo maana yake mkosaji aibebe yeye mwenyewe binafsi ili ajutie kosa lake.
 
Umeandika points kubwa mno hasa hapo kwenye rangi za bendera , yaani mama akiingilia wanasimba tunazimwaga cdm zote kila watu wawe bendera zinazosadifu vyama vyao
 
Unajua kuwa tayari Haji alikuwa na onyo kali kipindi kile ametozwa fine ya 5M akiwa simba 2020? Yeye nani kila mara awe anatozwa tu fine na anarudia makosa yale yale kisa ana uwezo wa kulipa fine?
 
Ni sawa naona kama Taifa tunahitaji default kwenye mpira wetu labda tutakuwa na heshima

Natamani tule Ban hata ya miaka 10 kwanza ili tukirudi tuwe na heshima na huu mpira katika kuuongoza
Sisi wengine hatutamani iwe hivyo, kama jinsi ambavyo nyinyi hamkutamani ligi ifungiwe wakati ambapo wengine walikuwa wanapewa hizo hukumu.
 
Kafatilie ligi ya Kenya uone ni nini kinaendelea kwasasa baada ya serikali yao kuingilia maswala la kimpira, huko FIFA, CAF na ulimwengu soka mtu kama SSH au kiongozi yoyote wa taifa (hasa Tz ambayo ni takataka tu kiuchumi) wanaonekana vinyeo tu na hawawezi kukoromeana na FIFA hata siku moja.

Huu mpira sio wenu, mpira ni wa wazungu na FIFA yao kwahiyo wao hata kuufingia mchezo wote wa mpira hapa Tz wanaweza na hakuna RAIS au kima yoyote yule anaeweza kupingana nao.
 
Mkuu walikuwa wanamfahamu vizuri Sana Yule mzee alikuwa c mtu wa kuingilika kirahisi hata huyo mstaafu wao analijua Hilo.

Mbona Kuna watu waliwahi kufungiwa akina mbwana makata, Na wengne Yule wa biashara United, Sasa manara ni Nani yeye yupo juu ya mfumo Na Sasa TFF isipoonesha nguvu yake kwenye hili Basi soka letu linaenda kufa Na king'amuzi Cha Azam nitatupa Na kubaki Na DStv kwa ajili ya kuangalia mpira wa nje tu

Kwa hyo viongozi wa timu kubwa wakikosea wasiguswe Ila Hawa wa timu ndogo hata wapigwe ban ya maisha sawa!
 
Haya ndio madhara ya Mpira kuongozwa na wapumbavu hapa nchini

Naitamani sana Ban ya FIFA kwenye mpira wetu
 
Siyo hofu bali ni fact Serikali ikiingilia maamuzi ya vyombo husika vya soka FIFA watatupiga tofali.
Kama viongozi hawatendi haki ni heri tu kufungiwa kuliko watu waishi kwa kuwaabudu.

Hofu ya kufungiwa isiwafanye watu wakashindwa kuusimamia ukweli.
 
Manara ni wa kwanza kufungiwa? Mbona hujawahi kushauri hili katika hukumu za wengine ?
 
Hawa ni majuha haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…