Wazee wanatoa maazimio yao juu ya kilichotokea tarehe 29 Oktoba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

MAAZIMIO YA MAZUNGUMZO YAWAZEE KUHUSU UJENZI WA AMANI, UMOJA NA HAKI NCHINI

TAREHE: 22 JANUARI 2026
MAHALI: DARES ES SALAAM, UKUMBI WA
MWALIMU NYERERE FOUNDATION

Imewasilishwa na:
Mzee Joseph W. Butiku, M/Kiti Bodi ya Wadhamini,Mwalimu Nyerere Foundation (MNF).

Kny. WAZEE
"HEKIMA, UMOJIA NA AMANI HIZI NI NGAO ZETU"

Utangulizi
Sisi Wazee, katika MAZUNGUMZO kwa uraghibishi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, tulisikitishwa na tunatoa pole kwa Watanzania wote, hususan waliofikwa na madhira yaliyotokana na uvunjifu wa amani uliosababisha vifo na uharibifu wa mali, siku ya na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Hali hiyo ilitokea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kwamba hadi sasa tunasubiri taarifa kamili ya usuli wa vurugu na ghasia na pia madhara halisi kwa uhai, mali na miundombinu ya umma na binafsi.

Pamoja na hayo, matukio ya ama Watu kutekwa, kupotea au kuuwawa nayo yameacha hofu kubwa kwa Wananchi na yameathiri misingi ya amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu.

Yameathiri jitihada za Wananchi kutumia fursa za kiuchumi na ajira kwa maendeleo yao nanchi yao. Hivi sasa kunachembechembe za migawanyiko na kushutumiana hususani katika mikabala kidini na kisiasa, jambo lisilo na afya katika ustawi na maendeleo ya nchi.

Kwa hekima, tunatoa maazimio yafuatayo:-

1. Kuhusu Maafa na Uharibifu
• Sisi Wazee tunatambua kuwa wote tuko katika maombolezo ya misiba ya kuondolewa uhaiwa wapendwa wetu. Pasipo kuwa na taarifa kamili, ni busara tuendelee kuwa watulivu na wenye subira. Tulisikitishwa, tunaomboleza na tunazifariji familia zote husika.

• Tunapendekeza Wananchi kuwa na subira wakati Tume ya Uchunguzi inaendelea
kutekeleza hadidu zao za rejea, kisha Serikali itoe taarifa kamili ndani ya muda muafaka kwa uwazi kuhusu Vifo na Mali zilizoharibiwa.

• Itakapowezekana, Serikali yaweza kuandaa pole (ubani) kwa waliofiwa na kutoa misaada wa kiafya na kisaikolojia kwa wahusika wote.

2. Kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

• Kama alivyoahidi Rais Bungeni, uanzishwe tena, mchakato jumuishi, huru na wazi wa mabadiliko ya Katiba, ukihusisha vyama vyote na makundi mbalimbali ya Wananchi

• Mchakato uwe na ratiba itakayohitimishwa kwa kura ya Maoni ya Wananchi (Referendum)

• Wananchi wote tushiriki kikamilifu maana Katiba ndio Sheria Mama na Dira ya namna
tunavyotaka kuishi na kujiongoza.

3. Kuhusu Uzalendo, Haki na Uwajibikaji

• Kila Mtanzania atangulize maslahi ya Taifa juu ya ubinafsi, uchama au makundi yoyote

• Viongozi wawajibike kwa matendo yao, kuwe na uwazi wa rasilimali na mifumo madhubuti ya usimamizi na udhibiti inayofanya kazi ipaswavyo.

• Serikali iendelee kusimamia haki na usawa wa raia, ikiwemo kuendelea kuwaachia kupitia taratibu za kisheria wafungwa/mahabusu waliokamatwa kwa sababu za kisiasa

4. Ujenzi wa Amani, Utatuzi wa Migogoro na Maridhiano

• Tunatambua kuwa katika nchi yetu, tunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira na kipato kidogo hususani kwa Vijana jambo ambalo ni kero. Sisi Wazee kama Wazazi wa Vijana hao, tunao wajibu wa kuwalea Vijana wetu katika njia zipaswazo na kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana na tatizo hili la kidunia ipaswavyo.

Wakati tunashughulikia kero hii na nyingine zozote, tunashauri kuwa na busara katika uwasilishwaji wa kero na kamwe tusikubali kushawishika kutengeneza mazingira ya nchi kutotawalika maana uzoefu umeonesha kuwa madhara yake ni mabaya zaidi na huwa ya kujirudia. Aidha chaguo la matumizi ya lugha chafu na matusi huzaa chuki na adhabu badala ya kutatua tatizo lililopo.

Sisi wazee tunaamini Watanzania hatujapoteza uwezo wa kutambua changamoto zetu, wala hatujapoteza uwezo wa kuzungumza kwa uhuru, utulivu, kuaminiana na umoja kutatua kero zinazotukabili. Hivyo, tunasisitiza kusikiliza malalamiko; kufanya mazungumzo, kutatua migogoro na taratibu za usuluhishi wa kweli kuliko maandamano ya vurugu au yasiyokoma.

• Tunapendekeza kuwa, Tume ya Maridhiano itakapoundwa, iwe na uwakilishi wenye mawanda mapana ya Wajumbe wenye Hekima, Uadilifu na Uzalendo usioshaka ikiongozwa na Raia anayestahiki asiyehusika kuongoza upande wowote wa kisiasa.

• Kila mtu ajiepushe na akemee matamko na vitendo vya kibaguzi au vinavyo hamasisha ubaguzi wowote, uwe wa kidini, kisiasa, ukabila, rika, hali ya uchumi, n.k

HITIMISHO: Tunatoa wito kwa Watanzania wote:
Kuwajibika na kuwawajibisha wasiowajibika kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni ziongozazo.

Kuweka maslahi ya Taifa juu ya Ubinafsi, Vyama wala Makundi yoyote.

Kushirikiana kwa umoja katika kutatua changamoto na migogoro kwa amani.

Mungu ibariki Tanzania, Watu wake na Urithi wao.
Asanteni
 
Haipatikani ie YouTube haiongei. Leta version ya kutoa sauti
 
Sina imani na wazee wengi wa Tanzania. Waulizwe walikuwa wapi wakati mambo ya kijinga yanafanyika.

Hawa wenyewe wamepangwa, kauli ni moja tu muuaji achukuliwe sheria kama wauaji wengine
Wao waliwashawishi vijana kufanya ujinga wa kuchoma moto vituo vya mafuta na maduka ya watu binafsi?.

Huyo unayemuita muuaji yupo kikatiba anaapishwa kikatiba, ukicheza na nguvu zake jiandae kukutana na adhabu nzito.
 
Screenshot_20260120-224356~2.png
 
MAAZIMIO YA MAZUNGUMZO YAWAZEE KUHUSU UJENZI WA AMANI, UMOJA NA HAKI NCHINI

TAREHE: 22 JANUARI 2026
MAHALI: DARES ES SALAAM, UKUMBI WA
MWALIMU NYERERE FOUNDATION

Imewasilishwa na:
Mzee Joseph W. Butiku, M/Kiti Bodi ya Wadhamini,Mwalimu Nyerere Foundation (MNF).

Kny. WAZEE
"HEKIMA, UMOJIA NA AMANI HIZI NI NGAO ZETU"

Utangulizi
Sisi Wazee, katika MAZUNGUMZO kwa uraghibishi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, tulisikitishwa na tunatoa pole kwa Watanzania wote, hususan waliofikwa na madhira yaliyotokana na uvunjifu wa amani uliosababisha vifo na uharibifu wa mali, siku ya na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Hali hiyo ilitokea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kwamba hadi sasa tunasubiri taarifa kamili ya usuli wa vurugu na ghasia na pia madhara halisi kwa uhai, mali na miundombinu ya umma na binafsi.

Pamoja na hayo, matukio ya ama Watu kutekwa, kupotea au kuuwawa nayo yameacha hofu kubwa kwa Wananchi na yameathiri misingi ya amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu.

Yameathiri jitihada za Wananchi kutumia fursa za kiuchumi na ajira kwa maendeleo yao nanchi yao. Hivi sasa kunachembechembe za migawanyiko na kushutumiana hususani katika mikabala kidini na kisiasa, jambo lisilo na afya katika ustawi na maendeleo ya nchi.

Kwa hekima, tunatoa maazimio yafuatayo:-

1. Kuhusu Maafa na Uharibifu
• Sisi Wazee tunatambua kuwa wote tuko katika maombolezo ya misiba ya kuondolewa uhaiwa wapendwa wetu. Pasipo kuwa na taarifa kamili, ni busara tuendelee kuwa watulivu na wenye subira. Tulisikitishwa, tunaomboleza na tunazifariji familia zote husika.

• Tunapendekeza Wananchi kuwa na subira wakati Tume ya Uchunguzi inaendelea
kutekeleza hadidu zao za rejea, kisha Serikali itoe taarifa kamili ndani ya muda muafaka kwa uwazi kuhusu Vifo na Mali zilizoharibiwa.

• Itakapowezekana, Serikali yaweza kuandaa pole (ubani) kwa waliofiwa na kutoa misaada wa kiafya na kisaikolojia kwa wahusika wote.

2. Kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

• Kama alivyoahidi Rais Bungeni, uanzishwe tena, mchakato jumuishi, huru na wazi wa mabadiliko ya Katiba, ukihusisha vyama vyote na makundi mbalimbali ya Wananchi

• Mchakato uwe na ratiba itakayohitimishwa kwa kura ya Maoni ya Wananchi (Referendum)

• Wananchi wote tushiriki kikamilifu maana Katiba ndio Sheria Mama na Dira ya namna
tunavyotaka kuishi na kujiongoza.

3. Kuhusu Uzalendo, Haki na Uwajibikaji

• Kila Mtanzania atangulize maslahi ya Taifa juu ya ubinafsi, uchama au makundi yoyote

• Viongozi wawajibike kwa matendo yao, kuwe na uwazi wa rasilimali na mifumo madhubuti ya usimamizi na udhibiti inayofanya kazi ipaswavyo.

• Serikali iendelee kusimamia haki na usawa wa raia, ikiwemo kuendelea kuwaachia kupitia taratibu za kisheria wafungwa/mahabusu waliokamatwa kwa sababu za kisiasa

4. Ujenzi wa Amani, Utatuzi wa Migogoro na Maridhiano

• Tunatambua kuwa katika nchi yetu, tunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira na kipato kidogo hususani kwa Vijana jambo ambalo ni kero. Sisi Wazee kama Wazazi wa Vijana hao, tunao wajibu wa kuwalea Vijana wetu katika njia zipaswazo na kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana na tatizo hili la kidunia ipaswavyo.

Wakati tunashughulikia kero hii na nyingine zozote, tunashauri kuwa na busara katika uwasilishwaji wa kero na kamwe tusikubali kushawishika kutengeneza mazingira ya nchi kutotawalika maana uzoefu umeonesha kuwa madhara yake ni mabaya zaidi na huwa ya kujirudia. Aidha chaguo la matumizi ya lugha chafu na matusi huzaa chuki na adhabu badala ya kutatua tatizo lililopo.

Sisi wazee tunaamini Watanzania hatujapoteza uwezo wa kutambua changamoto zetu, wala hatujapoteza uwezo wa kuzungumza kwa uhuru, utulivu, kuaminiana na umoja kutatua kero zinazotukabili. Hivyo, tunasisitiza kusikiliza malalamiko; kufanya mazungumzo, kutatua migogoro na taratibu za usuluhishi wa kweli kuliko maandamano ya vurugu au yasiyokoma.

• Tunapendekeza kuwa, Tume ya Maridhiano itakapoundwa, iwe na uwakilishi wenye mawanda mapana ya Wajumbe wenye Hekima, Uadilifu na Uzalendo usioshaka ikiongozwa na Raia anayestahiki asiyehusika kuongoza upande wowote wa kisiasa.

• Kila mtu ajiepushe na akemee matamko na vitendo vya kibaguzi au vinavyo hamasisha ubaguzi wowote, uwe wa kidini, kisiasa, ukabila, rika, hali ya uchumi, n.k

HITIMISHO: Tunatoa wito kwa Watanzania wote:
Kuwajibika na kuwawajibisha wasiowajibika kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni ziongozazo.

Kuweka maslahi ya Taifa juu ya Ubinafsi, Vyama wala Makundi yoyote.

Kushirikiana kwa umoja katika kutatua changamoto na migogoro kwa amani.

Mungu ibariki Tanzania, Watu wake na Urithi wao.
Asanteni

Without accountability, there can be no reconciliation!

While legal, criminal accountability usually requires a rigorous investigation process, political accountability can be, and often is, imposed immediately upon the evidence of mass killing. There’s no doubt that thousands of innocent civilians were killed or injured by security forces between October 29, 2025 and November 5, 2025. The evidence is overwhelming!
 
Hii ripoti ilikuwa imeshaandaliwa ndio maana wakaondoa mubashara ili isionekane kilichosemwa kwa wingi hakipo. Ni kama wanalazimisha tuwe na imani na tume ya mchongo.
 
Kilichoandikwa hakina tofauti na alichosema juzi,.alipotangaza kuitisha kikao.
 
Kabisa, ni kama ameenda kutakatisha hicho alichotumwa. Niliposikia tu wanaondoa mubashara, nikajua wanakwepa maoni halisi, wanataka kuweka ya viongozi waliofanya mauaji.
 
"HEKIMA, UMOJIA NA AMANI HIZI NI NGAO ZETU"
Hakuna HEKIMA mahali popote ndani ya hayo yaliyozungumzwa.
Neno HAKI haliwezi kuwa sumu likiandikwa au kutamkwa.
HEKIMA haiwezi kuwa ndiyo silaha ya kusafisha uchafu kwa watu waovu. Mnamfanyia kazi mtu asiye mzalendo; hekima itatoka wapi.

Wekeni hapo majina yenu mlioshiriki kwenye zoezi hili la kutaka kuwapumbaza waTanzania.

Maridhiano juu ya nini na nani?

Mtu aliyedhamiria toka mwanzo kuvuruga taratibu zote za HAKI ili abaki madarakani,; hizo HEKIMA zenu zilikuwa wapi kumwonya; na sasa mnashiriki uovu kwa kumtambua kuwa mtawala . Juhudi zenu ni mbinu hizo hizo alizotumia kubaki madarakani bila ya kuridhiwa na wananchi.

Wazee hamna Busara wala Hekima, na uzalendo wenu unamashaka, ni uzalendo wa maslahi.
 
Kabisa, ni kama ameenda kutakatisha hicho alichotumwa. Niliposikia tu wanaondoa mubashara, nikajua wanakwepa maoni halisi, wanataka kuweka ya viongozi waliofanya mauaji.
Huyu mzee Butiku kaamua kujichafua dakika za mwisho za uhai wake.

Waovu hawa Wametafuta tu njia ya kutumia jina la Mwalimu Nyerere kama juhudi za kujisafisha; lakini haitawezekana..
 
Back
Top Bottom