Wazee wanatoa maazimio yao juu ya kilichotokea tarehe 29 Oktoba

Wazee wanatoa maazimio yao juu ya kilichotokea tarehe 29 Oktoba

Endeleeni kujiliza humu humu mitandaoni mkitoka huko mitaani mtakutana na cha moto.
"Chamoto" unajuwa wazi kinawasubiri waovu mlioondoa uhai wa waTanzania ili muwe madarakani kwa mabavu. Haya yote unayajuwa; pamoja na kwamba tayari mtu kama wewe ni mzoga tayari hapo ulipo.
 
Huyo unayemuita muuaji yupo kikatiba anaapishwa kikatiba, ukicheza na nguvu zake jiandae kukutana na adhabu nzito.
Sasa utakataa vipi wewe kuwa ni mzoga tu, kwa haya unayoyaandika humu.
Ni binaadam gani mwenye uhai anayeweza kuandika maneno kama haya, na akaamini watu wenye akili timamu watamwelewa anachowasilisha?

Samia Suluhu Hassan hana nguvu tena; nguvu ni ya waTanzania; hata siku moja haiwezi kuwa ya mitutu ya kukodi.
Lakini wewe kama mzoga huwezi kuyajuwa haya.
Samia ni mzoga mwingine tarajiwa.
 
Endeleeni kujiliza humu humu mitandaoni mkitoka huko mitaani mtakutana na cha moto.
Screenshot_20260105-085755~2.png
 


MAAZIMIO YA MAZUNGUMZO YAWAZEE KUHUSU UJENZI WA AMANI, UMOJA NA HAKI NCHINI

TAREHE: 22 JANUARI 2026
MAHALI: DARES ES SALAAM, UKUMBI WA
MWALIMU NYERERE FOUNDATION


Imewasilishwa na:
Mzee Joseph W. Butiku, M/Kiti Bodi ya Wadhamini,Mwalimu Nyerere Foundation (MNF).

Kny. WAZEE
"HEKIMA, UMOJIA NA AMANI HIZI NI NGAO ZETU"

Utangulizi
Sisi Wazee, katika MAZUNGUMZO kwa uraghibishi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, tulisikitishwa na tunatoa pole kwa Watanzania wote, hususan waliofikwa na madhira yaliyotokana na uvunjifu wa amani uliosababisha vifo na uharibifu wa mali, siku ya na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Hali hiyo ilitokea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kwamba hadi sasa tunasubiri taarifa kamili ya usuli wa vurugu na ghasia na pia madhara halisi kwa uhai, mali na miundombinu ya umma na binafsi.

Pamoja na hayo, matukio ya ama Watu kutekwa, kupotea au kuuwawa nayo yameacha hofu kubwa kwa Wananchi na yameathiri misingi ya amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu.

Yameathiri jitihada za Wananchi kutumia fursa za kiuchumi na ajira kwa maendeleo yao nanchi yao. Hivi sasa kunachembechembe za migawanyiko na kushutumiana hususani katika mikabala kidini na kisiasa, jambo lisilo na afya katika ustawi na maendeleo ya nchi.

Kwa hekima, tunatoa maazimio yafuatayo:-

1. Kuhusu Maafa na Uharibifu
• Sisi Wazee tunatambua kuwa wote tuko katika maombolezo ya misiba ya kuondolewa uhaiwa wapendwa wetu. Pasipo kuwa na taarifa kamili, ni busara tuendelee kuwa watulivu na wenye subira. Tulisikitishwa, tunaomboleza na tunazifariji familia zote husika.

• Tunapendekeza Wananchi kuwa na subira wakati Tume ya Uchunguzi inaendelea
kutekeleza hadidu zao za rejea, kisha Serikali itoe taarifa kamili ndani ya muda muafaka kwa uwazi kuhusu Vifo na Mali zilizoharibiwa.

• Itakapowezekana, Serikali yaweza kuandaa pole (ubani) kwa waliofiwa na kutoa misaada wa kiafya na kisaikolojia kwa wahusika wote.

2. Kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

• Kama alivyoahidi Rais Bungeni, uanzishwe tena, mchakato jumuishi, huru na wazi wa mabadiliko ya Katiba, ukihusisha vyama vyote na makundi mbalimbali ya Wananchi

• Mchakato uwe na ratiba itakayohitimishwa kwa kura ya Maoni ya Wananchi (Referendum)

• Wananchi wote tushiriki kikamilifu maana Katiba ndio Sheria Mama na Dira ya namna
tunavyotaka kuishi na kujiongoza.

3. Kuhusu Uzalendo, Haki na Uwajibikaji

• Kila Mtanzania atangulize maslahi ya Taifa juu ya ubinafsi, uchama au makundi yoyote

• Viongozi wawajibike kwa matendo yao, kuwe na uwazi wa rasilimali na mifumo madhubuti ya usimamizi na udhibiti inayofanya kazi ipaswavyo.

• Serikali iendelee kusimamia haki na usawa wa raia, ikiwemo kuendelea kuwaachia kupitia taratibu za kisheria wafungwa/mahabusu waliokamatwa kwa sababu za kisiasa

4. Ujenzi wa Amani, Utatuzi wa Migogoro na Maridhiano

• Tunatambua kuwa katika nchi yetu, tunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira na kipato kidogo hususani kwa Vijana jambo ambalo ni kero. Sisi Wazee kama Wazazi wa Vijana hao, tunao wajibu wa kuwalea Vijana wetu katika njia zipaswazo na kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana na tatizo hili la kidunia ipaswavyo.

Wakati tunashughulikia kero hii na nyingine zozote, tunashauri kuwa na busara katika uwasilishwaji wa kero na kamwe tusikubali kushawishika kutengeneza mazingira ya nchi kutotawalika maana uzoefu umeonesha kuwa madhara yake ni mabaya zaidi na huwa ya kujirudia. Aidha chaguo la matumizi ya lugha chafu na matusi huzaa chuki na adhabu badala ya kutatua tatizo lililopo.

Sisi wazee tunaamini Watanzania hatujapoteza uwezo wa kutambua changamoto zetu, wala hatujapoteza uwezo wa kuzungumza kwa uhuru, utulivu, kuaminiana na umoja kutatua kero zinazotukabili. Hivyo, tunasisitiza kusikiliza malalamiko; kufanya mazungumzo, kutatua migogoro na taratibu za usuluhishi wa kweli kuliko maandamano ya vurugu au yasiyokoma.

• Tunapendekeza kuwa, Tume ya Maridhiano itakapoundwa, iwe na uwakilishi wenye mawanda mapana ya Wajumbe wenye Hekima, Uadilifu na Uzalendo usioshaka ikiongozwa na Raia anayestahiki asiyehusika kuongoza upande wowote wa kisiasa.

• Kila mtu ajiepushe na akemee matamko na vitendo vya kibaguzi au vinavyo hamasisha ubaguzi wowote, uwe wa kidini, kisiasa, ukabila, rika, hali ya uchumi, n.k

HITIMISHO: Tunatoa wito kwa Watanzania wote:
Kuwajibika na kuwawajibisha wasiowajibika kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni ziongozazo.

Kuweka maslahi ya Taifa juu ya Ubinafsi, Vyama wala Makundi yoyote.

Kushirikiana kwa umoja katika kutatua changamoto na migogoro kwa amani.

Mungu ibariki Tanzania, Watu wake na Urithi wao.
Asanteni

Kwani wazee ndiyo walioandamana October 29 !? Mbona wanajipa umuhimu kwa mambo ambayo hayawahusu.
Useless kabisa 🚮🚮
 
Kwani wazee ndiyo walioandamana October 29 !? Mbona wanajipa umuhimu kwa mambo ambayo hayawahusu.
Useless kabisa 🚮🚮
Wazee wanaheshimiwa siku zote afrika. Wewe utakuwa dogo wa Gen Z hamuelewi maana na umuhimu wa watu wanaowazidi umri kwenye maisha yenu.

Mmekuwa mnachezea simu za smartphone maisha yenu yote, hamjafundishwa kuhusu heshima kwa wazee au watu wenye kuwazidi umri.
 
Wazee wanaheshimiwa siku zote afrika. Wewe utakuwa dogo wa Gen Z hamuelewi maana na umuhimu wa watu wanaowazidi umri kwenye maisha yenu.

Mmekuwa mnachezea simu za smartphone maisha yenu yote, hamjafundishwa kuhusu heshima kwa wazee au watu wenye kuwazidi umri.
Wazee wapumbafu tu hao mbona hawakuishauri Serikali isiue waandamanaji tarehe 29 October!? Walikuwa kimya wakati Serikali inafanya mauaji hayo, Sasa hivi mambo yamekuwa magumu kwa Samia wametoka mafichoni.
Usanii na njaa zinawasumbua hamna hekima Wala busara wote ni majizi tu ya Samia.
 
Ukisha chukua pesa ya watu, lazima uwatumikie. Butiku kala pesa ndefu(1B) sasa anatafuta kuonyesha kafanya kazi. Hatutaki ulaghai wa Butiku na CCM.
 
Wazee wapumbafu tu hao mbona hawakuishauri Serikali isiue waandamanaji tarehe 29 October!? Walikuwa kimya wakati Serikali inafanya mauaji hayo, Sasa hivi mambo yamekuwa magumu kwa Samia wametoka mafichoni.
Usanii na njaa zinawasumbua hamna hekima Wala busara wote ni majizi tu ya Samia.
Wapumbavu ni vijana wenyewe waliokubali kudanganywa na kina Mange na Maria kwamba nyinyi ingieni barabarani huko mtakutana na JWTZ walio upande wenu!, ule ndio upumbavu wa kiwango cha lami kudhani kwamba wanajeshi wanaoapa mbele ya Rais watakuwa upande wa vijana wa Gen Z.

Hao wazee hawakuhusika katika kuwadanganya hao vijana waingie mtaani, ni ukosefu wao wa uelewa uliowadanganya. Wazee wakati huo walikuwa wamejifungia ndani.

Vijana mlileta uhuni serikali ikashughulika na nyinyi kihuni vile vile!. Huwezi kuwakwepa wazee mahali popote pale.

Tena usidanganyike na nguvu za ujana ulizonazo, muda hauna rafiki yoyote wenyewe unakimbia kwa kasi kila sekunde. Ukifumba ukifumbua na wewe tayari umeshakuwa mzee.
 
Hawa ni wazee au wazembe?🤔

Uzuri tulishaambiwa kuna wapuuzi watatumwa kama wazee kuja kuleta maridhiano na kufunika kombe mwanaharamu apite. Yameanza kutimia sasa.

Hivi kwa mfululizo wa matukio yaliyotokea kweli kama raia tuwatazame waliotenda uhalifu kama binadamu timamu wa kawaida badala ya wendawazimu,vichaa ,wavuta bange,na wakosa utu?🤔

Hawa wazembe wanataka sisi tushikane mikono na wauwaji na mashetani ili kuficha nini au kutetea nini?🤔

Wao kama alijitoa ufahamu kufanya waliyofanya then jibu ni moja tu ,"SHERIA IFUATE MKONDO NA ADHABU ZITOLEWE,HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA TANZANIA".

Sheria zikiendelea kubakwa then watawajibishwa na vyombo vya kimataifa kwa nguvu na shinikizo adhabu lazima wapewe shenzi kabisa. Tena mkome kutuzoea.
 
Hawa ni wazee au wazembe?🤔

Uzuri tulishaambiwa kuna wapuuzi watatumwa kama wazee kuja kuleta maridhiano na kufunika kombe mwanaharamu apite. Yameanza kutimia sasa.

Hivi kwa mfululizo wa matukio yaliyotokea kweli kama raia tuwatazame waliotenda uhalifu kama binadamu timamu wa kawaida badala ya wendawazimu,vichaa ,wavuta bange,na wakosa utu?🤔

Hawa wazembe wanataka sisi tushikane mikono na wauwaji na mashetani ili kuficha nini au kutetea nini?🤔

Wao kama alijitoa ufahamu kufanya waliyofanya then jibu ni moja tu ,"SHERIA IFUATE MKONDO NA ADHABU ZITOLEWE,HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA TANZANIA".

Sheria zikiendelea kubakwa then watawajibishwa na vyombo vya kimataifa kwa nguvu na shinikizo adhabu lazima wapewe shenzi kabisa. Tena mkome kutuzoea.
Hivyo vyombo vya kimataifa vina mengi mno ya kufanya, usidhani haki unastahili kuipata wewe peke yako.

Ukidhani una haki ya kuchoma moto nchi nzima tambua lipo jeshi la polisi pia lina haki ya kushughulika na wewe mleta fujo unayedhani una haki.

Mjifunze kuheshimu mamlaka zilizopo, mkijifanya vichwa ngumu mtakutana na vichwa ngumu kuwazidi nyinyi.
 
Huu muda wa kupoteza kwenye harakati kumbukeni kuna mamia ya wawekezaji wanakuja nchini wakitafuta wabia wazalendo wafanye nao biashara kwenye sekta ya viwanda.

Hao wakushirikiana nao kumbe mpo humu mnajaza vibonzo vya uanaharakati badala ya kuchangamkia fursa zinazokwenda kwa vijana wa mataifa mengine.
FB_IMG_1748360197313.jpg
 
Back
Top Bottom