Wazee wapenda taarifa ya habari ni wambea sana

Wazee wapenda taarifa ya habari ni wambea sana

Ni kuwa wazee wengi huwaambii kitu kuhusu taarifa ya habari. Kipindi chake pendwa kwenye TV ni taarifa ya habari. Ukweli ni kuwa mapenzi yote ya taarifa ya habari ni sababu ya umbea na majungu tu.

Anataka akifika kazini apate cha kusimulia wenzake. Waziri fulani hivi, mbunge fulani vile. Unakuta dingi ikifika muda wa taarifa ya habari anasimamisha kila kitu ili asikie majungu na kesho akawasimulie wenzake kazini

Ipo hivi. Wamama tunaowashutumu umbea na wapiga majungu huwa wanafanya hivyo kwenye level za mtaa. Yaani wanakuwa na habari za mtaani juu ya nani anatembea na nani, nani kamkopa nani, nani na nani haviivi, mtoto wa fulani hivi nk.

Madingi umbea wao ni level za kitaifa na kimataifa. Waziri fulani hivi, Saddam kamjibu Bush, mbunge kakiwasha nk nk. So madingi wapenda taarifa za habari ni wambea na watu wa majungu kama tu wamaza wambea wa kitaa.

Ukiona dingi anafuatilia taarifa za habari kwa karibu fahamu kuwa hamna kitu kingine zaidi ya kupenda umbea na majungu.
Kwahyo mnatusema wazee si ndio hili taifa kweli Lina potea kwa vijana kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom