Wazee wetu waliishi miaka mingi sana sababu walioa wake wengi

Wazee wetu waliishi miaka mingi sana sababu walioa wake wengi

Tawile
JamiiForums1876951498.jpg
 
Ukifanya utafiti chanzo cha vifo vya mapema vya wanaume wengi ni stress za ndoa.

Mwanamke mmoja ukiishi nae anakuzoea anakuona sawa na mtoto mwenzake.

Majukumu ya nyumba wanaachiwa wadada wa Kazi, hata ukizeeka Wana ungana na watoto kuwa kitu kimoja baada ya kuwalisha sumu, hawatambui mchango wako ulivyo jinyima Ili wao wale wasome.

Zamani wazee walijua siri akikuzingua bi Mkubwa walikuwa awatoi talaka kimya kimya anaenda kwa bi mdogo huko napo akivurugwa uenda kwa Mdogo zaidi akivurugwa huko urudi kwa Mkubwa ambae anakuwa amemmiss mme wake KWA mzunguko huo huo.

Hii iliwasaidia Sana wasife mapema na maradhi ya moyo, au kuuana kisa mapenzi. Thus walifika hadi miaka 100 kwa amani afya tele.

Ni mzigo mzito Sana kuubeba mzigo wa malezi mabovu ya mwenzako wako.

Mzazi anamlea binti vibaya madhara anaenda pata atakaeishi nae kifuatacho ni stress, umasikini, stroke, kisukari, kupooza nk.

Men die too young
Naunga mkono hoja wazazi wanalea vibaya mabinti zao halafu shida tunapata sisi tunaoenda kuoa,unakuta binti haambiliki,hatambui majukumu yake kama mke, zaidi anakuja kwako kufanya malumbano kwa kivuli cha ndoa.
 
Wanaume wa sasa baadhi yenu unakuta kabinti kamoja tu tena ka chuo kanafanya mtu atake kujiua, kutwa kulia lia humu na ukute kuna visenti aligharamia ndiyo wanadata, hao wanne si ndiyo mtachanganyikiwa kabisa na hivi mpo wachache mno siku hizi, heeeh' tutabaki na nani..!!?
Tena kibinti cha mwaka 2000
 
Naunga mkono hoja wazazi wanalea vibaya mabinti zao halafu shida tunapata sisi tunaoenda kuoa,unakuta binti haambiliki,hatambui majukumu yake kama mke, zaidi anakuja kwako kufanya malumbano kwa kivuli cha ndoa.
Halafu huwa malaika kabla ya ndoa akishapata tu cheti cha ndoa na mtoto hakuna rangi utoona.
Kazi na ndoa huwa havizoeleki,ukizoea ndoa kifuatacho ni talaka, ukizoea Kazi kifuatacho ni kufukuzwa Kazi.
Ukifukuzwa Kazi, ukipewa talaka kwa upumbavu wako unaenda kuwa mteja wa mitume na manabii wa uongo baada ya kumnenepesha Sana mganga.
 
Sahii kabisa
Ukiwa na matala
Stress za ndoa hutoziskia
Watashindana wao kwa wao
 
Mbona Mwinjilisti Reinhard Bonnke aliishi na kufa akiwa na miaka 79 akiwa na mke mmoja?
Billy Graham ameishi zaidi ya miaka 80 akiwa na mke mmoja.
Nilichokuja kugundua ni kwamba Hawa walimshirikisha Mungu kwenye suala la ndoa ndo maana wakapata wenzi sahihi.
Mi nafikiri suala ni kumuomba Mungu tu umpate aliye sahihi,kuoa wake wengi sio solution,unaweza ukawa na wanne wakakuvuruga kichwa kabisa,na ukawa na mmoja na akakutuliza
 
Mbona Mwinjilisti Reinhard Bonnke aliishi na kufa akiwa na miaka 79 akiwa na mke mmoja?
Billy Graham ameishi zaidi ya miaka 80 akiwa na mke mmoja.
Nilichokuja kugundua ni kwamba Hawa walimshirikisha Mungu kwenye suala la ndoa ndo maana wakapata wenzi sahihi.
Mmh, kama ni sahihi mbona Gets kaachana na mkewe
 
Hivi ukishaishi miaka 100 then ufe inakusaidia nini?
 
Back
Top Bottom