Waziri aagiza dereva wa gari aliyemgomea trafiki anyang'anywe leseni

Waziri aagiza dereva wa gari aliyemgomea trafiki anyang'anywe leseni

Hizi ni nyakati za UNANIJUA Mimi Nani?

Kwamba huyo traffic hawezi kumwambia dereva chochote.

Ukishakuwa na genge la hivyo, ni jambo hatari.

Leo unafurahi Kwasababu limeanzia kwa traffic, lakini Kama huyo jamaa amemfanyia hivyo traffic police maana yake anaweza kumfanya hivyo RAIA yeyote anayetumia barabara na asifanywe kitu.
 
Hivi trafiki ndo anatakiwa asimamishe magari hivyo, kwamba anayazuia magari yasiyokubali kusimama kwa mikono? Labda huyo dereva ana tatizo kweli au amekuwa frustrated hawezi kukanyaga mafuta na kumjeruhi? ni muhimu weledi utumike kwenye kufanya kazi... na huenda ni usumbufu usio na maana mnaosababishia watu kwa kuendekeza rushwa kunafanya wengine wana behave namna hii.

Msijione watakatifu.​
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video fupi akiendelea kuendesha gari aina ya Nissan huku mbele yake kukiwa na askari wa Usalama Barabarani.

Amesema “Apelekwe kwenye vyombo vya dola na leseni tuliyompa anyang’anywe kabisa, haiwezekani askari yupo kazini anakuzuia wewe unampelekea gari, nina wasiwasi na akili za madereva wetu sasa hivi, lazima atakuwa na shida mahali.”
Kwahiyo huyu Naibu waziri yeye amejipachika mamlaka ya mahakama?

Kuna watu bado hamjui hawa traffic wanavyozinguwa barabara ni.

Traffic wajanja walishajiongeza siku nyingi wanakomaa na Daladal, kirikuu na magari makubwa, hawana mpango na hizi private car zimewaponza wengi hawana kazi au wamehamishiwa Polisi huko, ukiona gari ni ya RPC au DC.

Kutoka Tunduma mpaka Sumbawanga huwezi kusimamishwa na traffic hata siku moja.
 
Kwamba pengine huwajui Traffic police wa Tanzania ! Hawa traffic police wanasimamisha Gari kwa lengo la kutafuta makosa kwa lengo la bulling wapate rushwa. Sasa kwa Akili ya kawaida huo ndo Utaratibu wa kusimamisha Gari? Kwa vyote vyote vile walishindwana katika hiyo bulling.
 
Kwamba pengine huwajui Traffic police wa Tanzania ! Hawa traffic police wanasimamisha Gari kwa lengo la kutafuta makosa kwa lengo la bulling wapate rushwa. Sasa kwa Akili ya kawaida huo ndo Utaratibu wa kusimamisha Gari? Kwa vyote vyote vile walishindwana katika hiyo bulling
 
Hizi ni nyakati za UNANIJUA Mimi Nani?

Kwamba huyo traffic hawezi kumwambia dereva chochote.

Ukishakuwa na genge la hivyo, ni jambo hatari.

Leo unafurahi Kwasababu limeanzia kwa traffic, lakini Kama huyo jamaa amemfanyia hivyo traffic police maana yake anaweza kumfanya hivyo RAIA yeyote anayetumia barabara na asifanywe kitu.
Kwa nini huyo traffic police asimamishe Gari kwa Utaratibu huo? Tatizo liko kwa huyo traffic police.
 
Dereva
alifanya ustaarabu sana mimi nakulima tairi kabisa ili nifutiwe reseni vizuri
 
Back
Top Bottom