Waziri aagiza dereva wa gari aliyemgomea trafiki anyang'anywe leseni

Waziri aagiza dereva wa gari aliyemgomea trafiki anyang'anywe leseni

Magari kama haya yawe tu yanaingia kwenye mikono ya serikali moja kwa moja, gari la hivi litaifishwe kabisa na kuwa gari la umma likasaidia kazi nyingine za maendeleo ya kitaoifa, kama trafiki kafanyiwa hivi, vipi bodaboda, vipi mtembea kwa miguu, huu ni utovu wa nidhamu na dharau, serikali chukueni hilo gari, ashike adaby katika maisha yake yote na iwe fundisho kwa wengine, hiyo ni maana kwamba alikusudia kumuua huyo trafiki.
Trafiki mwenyewe hajielewi, akili yote imekuwa paralized na rushwa kiasi kwamba hata maisha yake hathamini.

Mtumishi wa umma asiekuwa na weredi wa kazi hatima yake ni kifo tu.

Mpumbavu sana trafiki yule
 
tusibadilishe mada,
Kwa wale walipitia vyuo vya driving wanajua, taratibu za barabarani na mamlaka ya Traffik
1. Traffic anayo mamlaka Kisheria ya kusimamisha chombo cha moto kikiwa barabarani sehemu ambayo ni salama kwa sababu anazoona zina faa. Inaweza kuwa kucheki, Leseni na vifaa muhimu vinavyotakiwa kuwa kwenye gari, Hali ya chombo chenyewe, taa, matairi, break nk
2. Swala la kuwa alisimama wapi wakati anasimamisha sio hoja muhimu hapa japo inaweza kuja kama njongeza
Wacha kutetea ujinga na wewe. Kusukumana na gari inayotembea ni upumbavu sana na nikufanya kazi bila weredi.

Huyo trafiki nguvu bila akili
 
Hata swala kama hili mpaka waziri alizungumzie kweliii???
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video fupi akiendelea kuendesha gari aina ya Nissan huku mbele yake kukiwa na askari wa Usalama Barabarani.

Amesema “Apelekwe kwenye vyombo vya dola na leseni tuliyompa anyang’anywe kabisa, haiwezekani askari yupo kazini anakuzuia wewe unampelekea gari, nina wasiwasi na akili za madereva wetu sasa hivi, lazima atakuwa na shida mahali.”
tarafiki wengi wanasababisha wao kudharauliwa sababu ya kuenda 2000
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video fupi akiendelea kuendesha gari aina ya Nissan huku mbele yake kukiwa na askari wa Usalama Barabarani.

Amesema “Apelekwe kwenye vyombo vya dola na leseni tuliyompa anyang’anywe kabisa, haiwezekani askari yupo kazini anakuzuia wewe unampelekea gari, nina wasiwasi na akili za madereva wetu sasa hivi, lazima atakuwa na shida mahali.”
Tatizo liko kwa maaskari wetu, dereva anajua hana kosa lolote ila askari wanataka kumtia hela. Kumbe hata waziri hajui taasisi anayoiongoza. Tatizo la kupendelea wazanzibari na kuwapa kazi za watanganyika
 
Kwan sheria inasemaje? nchi haiwez kuwa inaendeshwa na mtazamo wa waziri, ni vzr sheria ikafata mkondo wake na waziri akasisitiza Hilo. Huku tunakoelekea sio pazur
 
Kwanza ukiona trafiki anahatarisha maisha yake utadhani anataka kupata medali, ujue ana shida fulani. Ni ujinga na upuuzi, unless hana familia inayomtegemea.

Kuna wakati mambo kama haya yanatokana na mtumishi husika (hapa trafiki) kuelekeza mambo ambayo ni mazuri kwa kutumia nguvu huku mteja akiwa hana habari. Wateja wachache (hapa dereva) wata act against hizi orders. Mfano trafiki anaweza badirisha njia ya magari, bila kutoa sababu, baadhi ya madereva watagoma, lakini kumbe mbele ya barabara anayowazuia kupita yeye anajua kumejaa maji n.k. Si ilikuwa rahisi kuwaambia piteni huku, kule mbele kumejaa maji?

Si kila kitu kiwe amri, hawa askari pia wafundishwe customer care wakiwa maeneo yao ya kazi, kwa sababu wanatoa huduma sawasawa na maeneo mengine tunakopata au kutoa huduma tukaishia kusifu au kuzipigia kelele. Watumiaji wa barabara ni wateja, ndio maana wanalipia kodi mbalimbali za vyombo vya moto na wanapaswa kupewa huduma bora na wadau watoao huduma. Off course kuna cases chache ambazo unahitaji kutumia nguvu, lakini tujiulize kama kungekuwa na mazungumzo mazuri mwanzoni, je hilo jambo lingetokea?

Karibu manyukano yote ya barabara kati ya trafiki na watumia barabara si ya vita au kuhujumu uchumi hadi trafiki awe tayari kuondoa uhai wake. Tuwe tunazungumza.
 
Askari wenyewe wajinga tu si angechukua usajili wa gari atemane na dereva. Haya mfano pale agongwe afe itakua imemsaidia nini
 
Wacha kutetea ujinga na wewe. Kusukumana na gari inayotembea ni upumbavu sana na nikufanya kazi bila weredi.

Huyo trafiki nguvu bila akili
Wengi si fomfoo felia watakuaje na akili hapo ni mwendo wa nguvu nyingi
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video fupi akiendelea kuendesha gari aina ya Nissan huku mbele yake kukiwa na askari wa Usalama Barabarani.
Siasa nyingi
Trafiki wajikaanga wenyewe kwa mafuta yao, hizo leseni wanatoa kwa rushwa na hayo ni baadhi ya matunda yake
 
Back
Top Bottom