Waziri Abdallah Ulega: Madai ya Samaki kuhifadhiwa kwa maji ya maiti ni hisia tu

Waziri Abdallah Ulega: Madai ya Samaki kuhifadhiwa kwa maji ya maiti ni hisia tu

Hii ndio Taarifa rasmi iliyotolewa na Naibu Waziri Abdalla Ulega bungeni Dodoma, kwamba uvumi wa samaki kuhifadhiwa kwa kutumia dawa za Maiti hauna ukweli na ni hadithi za kufikirika.

Sasa kama huu ndio Msimamo wa Serikali basi ATAFUTWE MTU ALIYEVUMISHA ILI ATUAMBIE ALIKOTOA UZUSHI HUO .
Hahaha
 
Makamu wa rais aliteleza sana kutoa kauli ile tayari ameshaua biashara ya samaki ,kwa hisia hizo hizo watu wamepata kinyaa cha kutumia hao samaki
Hata mimi sinunui tena samaki wa kanda ya ziwa😅😅
Lisemwalo lipo
 
Ukweli ni kwamba matukio kama hayo yamekuwepo tena kwa muda mrefu sana.

Na hii ndio ilipelekea hata Biashara ya mabucha ya Samaki mikoani ikaporomoka miaka kadhaa iliyopita.

Tatizo kubwa hapa ni Nafasi ya mtoa kauli "VP".
Ambaye ameitoa mbele ya hadhara tena mbele ya wataalamu wa Afya.

Yeye kwa mamlaka yake anayo nafasi ya kutoa amri kwa mamlaka husika za uhifadhi wa madawa hayoili, kuchukuliwa hatua za uzembe wa kuruhusu madawa hayo kuingia mikono isiyostahili.

Pia angehakikisha vyombo vya dola vinalikomesha jambo hilo mara moja.
Tena hiyo ingekuwa amri ya kimyakimya kwa vyombo vya usalama kufanya utekelezaji wake.

Sasa badala yake ametoka hadharani tena mbele ya vyombo vya habari na pia baadhi ya wataalamu wa kutoka nje.
Na kutoa kauli ile. . ....jambo ambalo linaweza kusababisha Madhara makubwa kwenye sekta ya viwanda vya Samaki vinavyosafirusha samaki toka ziwa Victoria nje ya nchi.

Wazungu hawakawiagi kutoa tamko la kuzuia vitu au chakula chochote wanachokihofia kwa usalama wa afya zao.
Afya huku kwetu La patrona so jambo la msingi saaana...!! Sisi tunatakiwe tuzaliwe tuishiishi tuu kama mifugo mingine, tuchinjwe au kufa kwa hiyari
 
Kwa Hapa dar,
Hakuna pa kuponea,labda mboga ulime kwako

Mchicha wa ubungo
unalimwa msewe kando kando ya mfereji unaotililisha maji taka toka mlimani campus na chuo Cha maji

Ule wa mabibo sokoni,
Mwingi unamwagiliwa na majitaka tiririka kutoka hostel za wanachuo

Ule wa temeke,
Unamwagiliwa na majitaka tiririka toka msd na kiwanda Cha madawa keko.

Ukienda tandale,tandika manzese,mbagala,g/mboto,mtoni mtongani, magomeni,m/chai,muhimbili huko Ndo balaaa na nusu.
Tena unawekewa booster..mbegu zinatupwa leo kwenye udongo,baada ya siku nne mchicha umekomaa.
 
Kwani ni maji ya kuoshea maiti au dawa ya kuhifadhia maiti??

Maana hii ni story ya muda sana.
wapuuz hao, heti maji yakuoshea maiti, sio aseme dawa za kuifadhia maiti, halafu ndio wasomi wetu hao,

We maji ya kuoshea maiti ,maiti Wengine wamekufa kwa ajali,maladhi ya aina mbalimbali na yanakuwa na mchanganyiko wa kinyesi na damu na uchafu mwingine, leo ukaifadhie samaki kweli?

Mimi wamenitia kinyaa kwanza sili Tena hao samaki, na washaharibu soko la hao Samaki sababu ya kukurupuka kwao
 
Wewe sangara wabichi wanasafirishwa kwa basi Kutoka Mwanza hadi Dar ndani ya visalfeti halafu unambishia VP?
Kwahiyo ndio wanaifadhiwa kwa maji ya kuoshea maiti zilikufa kwa ajali, kansa ya ini na kansa ya Koo, na zilikufa kwa maladhi mbalimbali, ndio maji yake yanatumika kuifadhia samaki?

Kwann anasema Ni maji yalibayokia baada yakuosha maiti na sio aseme hile dawa fomalin
 
Itasikitisha sana, endapo hizo taarifa zitakua na ukweli...
 
Back
Top Bottom