Point taken.Huyu Waziri naye ana upungufu mkubwa. Atawezaje kusema kuwa watanzania wapo salama wakati tunaambiwa kuwa 60% ya wagonjwa wote wa saratani wanatoka kanda ya Ziwa?
Yawezekana maji ya kuoshea maiti siyo chanzo cha hali hiyo, lakini kusema wakazi wa kanda ya ziwa wapo salama, ni uwongo. Linatakiwa lipatikane jibu, kwa nini wagonjwa wa saratani ni wengi sana kanda ya Ziwa kuliko maeneo mengine yote ya Tanzania?
Kwa sasa kila mwanachi achukue tahadhari kwa kuzingatia all hypotheses:
1) uhifadhi wa samaki kwa kutumia chemicals hatari (ulaji samaki wa ziwa Victoria ni hatari)
2) mercury poisoning (maji na vyakula vinavyopatikana maeneo ya machimbo ya wachimbaji madini wadogo ni hatari)
3) heavy metal contamination (maji na vyakula kutoka maeneo yaliyopo mazingira ya uchimbaji madini ni hatari)
4) madawa yanayotumika kwenye kilimo.cha pamba (ardhi inayotumika kwenye kilimo cha pamba ni hatari inapotumika katika kilimo cha mazao ya chakula).
5) utiririshaji wa maji ya sumu ndani ya ziwa kutoka viwandani (maji ya Ziwa Victoria ni hatari)
Chukua tahadhari mpaka sababu ya uhakika itakapopatikana. Utafiti wa jambo hili unaweza kuchukua miaka kadhaa mpaka kupata jibu la uhakika.