Waziri adaiwa kumwaga noti kununua Kawe beach, NHC yasema haijauzwa ni mali yake na kampuni ya Dubai

Sasa mpangaji tu unapewe 300m unagoma kuondoka kwani nyumba yako. Chota hela kajenge ghorofa ghoba au mbweni uhamie kwako achana nyumba za watu, kwani NHC akikupa notisi si unaondoka mikono mitupu. mi hata sijui wanalalamika nini
Kuna kitu nadhani hakijaelezewa wajuvi wa mambo waje watueleweshe vizuri.
Kwa uelewa wangu ni kuwa nyumba za NHC mpangaji ukikaa muda mrefu wanaweza wakakuuzia ile nyumba ila hawauzi ardhi. Utakaa hapo lakini ardhi bado inahesabika kuwa ya NHC.
Kwa hiyo mpangaji anahesabika kapanga kwenye ardhi japo nyumba ni yake ndio maana unaona mpangaji anapewa pesa ndefu.
 
Chai kama Chai.

Hizi chai zenu ziishie kwenye vijiwe vyenu wa kuchunga ng'ombe huko. Humu mnalidhalilisha jukwaa
 
Ueandika maneno meeengi, hata kapicha hamna!
Junguuuuz!
 
Ungeandika kitabu ungepata hela,ufisadi wa kuwekeza ni mzuri kuliko wa kuficha pesa china
 
Kwani sheria inaruhusu wageni kumiliki ardhi? inakuwaje hilo eneo limilikiwe na NHC na kampuni ya dubai........tutakuja jikuta nchi yote imeshapigwa mnada kwa wageni wanaoitwa wawekezaji.
 
Kuna watanzania wanaandikisha kampuni dubai kisha kuja kudhulumu raia wenzao kwa kujifanya wawekezaji kutoka nje.
Tulisikia wale TICTS tukiambiwa na waziri ni kampuni ya hongkong wakati sio siri kila mtu anajua wamiliki ni karamagi wa bukoba na yule mhindi wa dar subash patel. Binafsi nimemsikia karamagi akisema kwa kauli yake ticts ni yao.
Hata hili la bandari ni hila za wenyeji tu. Wao wanaweza kua wanashirikiana na DPW kuja kuweka ufalme wa dubai hapa nchini kwenye bandari zetu.
 
Kama unaogopa kumtaja Si ukae kimya tu
 
Taarifq nyeti ssna
Hakuna picha

Inaw3zekana watoa habari wana lengo la kublackmail mhusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…